Habari

  • ​KIWANDA KIKUBWA CHA KUCHAKATA SAMAKI KUJENGWA NCHINI

    November 27, 2023

    ​Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega amesema kufuatia sera nzuri za kuvutia uwekezaji za Serikali ya Mhe. Rais Dkt, Samia Suluhu Hassan zimeifanya Kampuni ya Albacora kutoka nchini Hispania kuja hapa nchini kujenga kiwanda kikubwa cha kisasa cha kuchaka samaki.

  • PROF. SHEMDOE: MAAFISA UGANI NDIO INJINI YA NCHI KUWA KAPU LA CHAKULA BARANI AFRIKA

    November 27, 2023

    Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Prof. Riziki Shemdoe amewataka Maafisa Ugani kutumia taaluma zao vizuri ili kusaidia kutimiza malengo ya Serikali ya Awamu ya sita inayoongozwa na Rais, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

  • ​MAAFISA UVUVI KAMATENI VIWANDA, MADUKA YANAYOUZA NYAVU HARAMU-MNYETI

    November 20, 2023

    Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Alexander Mnyeti amewataka maafisa uvuvi kote nchini kuhakikisha wanapita kwenye viwanda vya ndani na maduka yote yanayouza nyavu za kuvulia samaki zisizoruhusiwa na kuwachukulia hatua za kisheria badala ya kushughulika moja kwa moja na wavuvi wanaozitumia pindi zikiingia sokoni.

  • ​MNYETI ATANGAZA KIAMA CHA WAVUVI HARAMU ZIWA TANGANYIKA

    November 20, 2023

    Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Alexander Mnyeti ametangaza vita kwa watu wote wanaojihusisha na vitendo hivyo katika Ziwa Tanganyika ambapo ameweka wazi mipango ya Serikali kupitia Wizara yake kuunda kikosi kazi maalum kitakachoshughulikia jambo hilo.

.