Daktari wa mifugo asiye mtanzania (Foreigner) anasajiliwa vipi na Baraza.

i) Awe na shahada ya tiba ya mifugo.

ii) Awasilishe usajili wake toka mamlaka inayosimamia taaluma ya veterinari kutoka nchi anapotoka.

iii) Awe na kibali cha kufanya kazi hapa nchini kutoka mamlaka husika.

iv) Atatakiwa kulipa ada ya usajili ya US$ 500 na kulipia US$ 300 kila mwaka atakaokuwepo hapa nchini.