Vibali vya Uvuvi

Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Sekta ya Uvuvi) inatoa vibali vya kuruhusu usafirishaji wa samaki na mazao ya uvuvi. Kabla ya kupata vibali, mwombaji anatakiwa kutimiza vigezo na masharti yaliyoainishwa kwenye sheria, kanuni na miongozo ya uvuvi.

  • VIBALI VYA KUANZISHA UKUZAJI VIUMBE MAJI

Wizara ya Mifugo na Uvuvi - Sekta ya Uvuvi inatoa vibali vya kuruhusu kuanzisha ukuzaji viumbe maji hususani ufugaji wa samaki na ukulima wa mwani. Kabla ya kupata kibali muombaji anatakiwa kutimiza vigezo na masharti yaliyoainishwa kwenye sheria, kanuni, na miongozo ya ukuzaji viumbe maji.

  • VIBALI VYA KUINGIZA NCHINI PEMBEJEO NA ZANA ZA UKUZAJI VIUMBE MAJI

Wizara ya Mifugo na Uvuvi - Sekta ya Uvuvi inatoa vibali vya kuingiza nchini pembejeo na zana za ukuzaji viumbe maji. Kabla ya kupata kibali muombaji anatakiwa kutimiza vigezo na masharti yaliyoainishwa kwenye sheria, kanuni, na miongozo ya ukuzaji viumbe maji.

.