Utangulizi

Dawati la Sekta Binafsi lilizinduliwa tarehe 1/10/2018 na Mhe. Luhaga Joelson Mpina (Mb), Waziri wa Mifugo na Uvuvi na kuhudhuriwa na Viongozi na Watendaji wa Serikali, Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji, Taasisi za Fedha, Wadau wa Maendeleo na Sekta Binafsi.

Wadau tunaofanya nao kazi ni;

  1. ASPIRES --- Agriculture Sector Policy and Institutional Reform Strengthening
  2. DALBERG -- American Advisory Firm
  3. ANSAF ----- Agricultural Non State Actors Forum
  4. SAGCOT ---- Southern Agricultural Growth Corridor of Tanzania
  5. TADB ------ Tanzania Agricultural Development Bank

Lengo la kuanzishwa kwa Dawati la Sekta Binafsi

  1. Kutekeleza ahadi ya Mheshimiwa Rais, John Pombe Joseph Magufuli, wakati wa kampeni za uchaguzi za mwaka 2015 nabaada ya kuchaguliwa ya kufanya mageuzi makubwa katika Sekta ya Mifugo na Uvuvi.
  2. Kutekeleza ilani ya uchaguzi ya CCM ya 2015 ibara ya 25 (a – q) kwa upande wa mifugo na ibara ya 27 (a-p) kwa upande wa uvuvi.
  3. Kutekeleza Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka 5 (2016-2021) ambao umetoa vipaumble kwa mazao ya mifugo ambayo ni nyama ya ng’ombe, maziwa, kuku na ngozi. Kwa upande wa uvuvi ni uvuvi wa samaki katika mito na maziwa, uvuvi wa bahari kuupamoja na ufugaji wa samaki katika vizimba na mabwawa/madimbwi.
  4. Kutekeleza Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo Nchini Awamu ya Pili (ASDP II) na Mpango Kabambe wa Kuendeleza Sekta ya Mifugo (TLMP) ili kufanya mageuzi ya sekta hizi.

Majukumu ya Dawati la Sekta Binafsi

1.Kuwa daraja kati ya Serikali na Sekta Binafsi katika sekta za mifugo na uvuvi.

2.Kufanya uchambuzi wa kimkakati wa minyororo wa thamani kwa ajili ya kusaidia upatikanaji wa ushahidi na kupitia Blueprint ya Serikali na kuanisha maeneo yanayohitaji mabadiliko ya sera na sheria kwenye sekta za mifugo na uvuvi ili kuweka mazingira mazuri ya biashara.

3.Kuratibu na kufuatilia uwekezaji wa kwenye Sekta ya Mifugo na Uvuvi kwa kuwatambua wadau, kujua changamoto na kuzitatua.

4.Kutangaza fursa zilizopo kwenye sekta ya mifugo na uvuvi ikiwa ni pamoja na kuhamasisha uwekezaji wa viwanda.

5.Kushirikiana na wadau katika utafiti na ushauri wa masoko (Market Inteligency) kutathmini muelekeo wa bei za masoko ya ndani na nje kwa mazao ya Mifugo na Uvuvi.

6.Kuwaunganisha wadau na taasisi za kifedhakwa ajili ya mikopo na bima.

Mikopo na Dhamana

Huduma ya bima

Benki ya Posta Tanzania na Shirika la Bima la Taifa (NIC) wanaendelea na mchakato wa maandaliza ya utoaji wa bima ya mifugo na uvuvi ambayo itakuwa inatumika kama dhamana wakati wa uombaji wa mikopo. Kwa sasa NIC wapo kwenye hatua ya kusaini

treaty (Jan. 2020) ili kuendelea na taratibu za upatikanaji ya huduma ya bima.

Dhamana za TADB

Kwa upande wa dhamana ya TADB kupitia dhamana ya AGF ambayo inadhamini asilimia 50 ya dhamana bado haijaweza kutumiwa na wafugaji na wavuvi hivyo maongezi yanaendelea juu ya kuboresha huduma hii. Kikao cha mwisho kilifanyika tarehe 21/01/2020

Dhamana za PASS

Kwa upande wa PASS juhudi tunaendelea kuwaunganisha wadau wenye changamoto ya dhamana ikiwa pamoja na Ushirika wa watengenezaji wa bidhaa za Ngozi (TALEPA) na vyama vya ushirika wa maziwa Tanga (TDCU).

Mfano wa utaratibu wa dhamana ya PASS kwa mkopaji wa million 500 ambao hutoa asilimia 60 ya dhamana ni kama inavyoonekana kwenye jedwali namba 2 hapa chini Jedwali Na. 2 Utaratibu wa dhamana ya PASS

Kiasi cha mkopo

500,000,000.00

0.13

Makato

Gharama za kuomba (Application fee)

0.625%

500,000,000

3,125,000.00

Gharama za andiko la biashara

1.300%

500,000,000

6,500,000.00

Gharama ya dhamana (Quarantee fee (after loan approval)

1.300%

500,000,000

6,500,000.00

Riba (Interest fee (pa reducing))

13.000%

500,000,000

65,000,000.00

Dhamana

500,000,000.00

325,000,000.000

325,000,000.00

Mchango wa mkopaji 65%

Kiasi cha mkopo

500,000,000.00


Lease financing (EFTA)

Wakopaji wa vifaa/pembejeo vya mifugo na uvuvi wanaweza pata zana kupitia mikopo ya EFTA ambapo hulipa malipo ya awali ya asilimia 20 hadi 30 na kifaa kilichonunuliwa hutumika kama dhamana.

Tunaendelea kuunganisha wadau wenye mahitaji hususani wale wenye changamoto ya dhamana na wanahitaji vifaa.

Kufuatilia hali ya mikopo ya wafugaji na wavuvi kwenye taasisi za fedha;

Katika kipindi cha Oktoba 2018 hadi Januari 2020 jumla ya mikopo ya mifugo na uvuvi imefikia Tshs. Bil. 104.46 ambayo ipo kwenye hatua tofauti. Mikopo iliyotolewa na kupitishwa (Approved) ni Tshs. Bil 26.15 (bilioni 23.5 mifugo na bilioni 2.6 Uvuvi) na mikopo iliotolewa ni Tshs bilioni 12 (bilioni 11.7 Mifugo na milioni 323.8 Uvuvi).



.