Daktari wa mifugo asiye Mtanzania anaweza kusajiliwa na kufanyakazi hapa nchini? (Temporary and permanent registration)?

i) Daktari asiye Mtanzania anaweza kusajiliwa na kufanya kazi kama za utafiti, kama mtaalam muelekezi, mkufunzi, na wenye ujuzi maalum kwa muda maalum (Temporary registration).

ii) Daktari asiye Mtanzania anaweza kusajiliwa na kufanya kazi za uwekezaji katika tiba ya afya ya wanyama kwa masharti ya kufanya kazi kwa muda wote kwa kushirikiana na madaktari wazawa (Permanent registration).