Baraza la Veterinari Tanzania

Baraza la Veterinari Tanzania lilianzishwa kwa mujibu wa kifungu cha 3 cha Sheria ya Veterinari Na. 16, ya Mwaka 2003 baada ya kufuta Sheria ya Madaktari Wapasuaji wa Wanyama (CAP 376) ya Mwaka 1958, na majukumu yake ni kusimamia taaluma ya veterinari na huduma za afya ya wanyama ili kuhakikisha kuwa wafugaji wanafaidika na mifugo yao.

Majukumu ya Baraza

Majukumu ya Baraza yameaanishwa katika kifungu cha 5 cha Sheria ya Veterinari Na. 16, ya Mwaka 2003 ambayo ni pamoja na;
a. Kusajili, kuorodhesha na kuandikisha wataalam, wataalam wasaidizi na kusajili vituo vya huduma ya afya ya wanyama;
b. Kumshauri na kutoa mapendekezo kwa Mhe. Waziri kuhusu jambo lolote linarohusu utaoji huduma za afya ya wanyama;
c. Kusimamia maadili na mienendo ya wataalam;
d. Kuweka sifa za mafunzo ya taaluma ya veterinari, vyuo na taasisi zinazotoa mafunzo ya wataalam wa afya ya wanyama;
e. Kusimamia huduma ya tiba ya wanyama;
f. Kushirikiana na taasisi zingine kutambua mitaala katika taaluma ya veterinari; Kuweka viwango vya huduma ya tiba ya wanyama, mipaka ya kutoa huduma kwa ngazi mbalimbali za wataalam wa afya ya mifugo na viwango kwa masomo yanayohusu taaaluma;
g. Kuhamasisha maendeleo ya taaluma ya tiba ya wanyama;
h. Kutunza na kutoa taarifa zinazohusu taaluma ya tiba ya wanyama;
i. Kuandaa mitihani ya taaluma kwa ajili ya usajili, kuandikishwa na kuorodheshwa;
j. Kufuatilia utendaji kazi wa madaktari, wataalam wasaidizi na wasaidizi wa wataalam wa mifugo;na
k. Kutekeleza jambo lolote jingine kwa mujibu wa Sheria.

USAJILI

Baraza la Veterinari husajili, kuandikisha na kuorodhesha wataalam wa kada mbalimbali za taaluma ya mifugo kulingana na vigezo vifuatavyo:-

USAJILI WA MADAKTARI WA MIFUGO

  1. Awe na Shahada ya udaktari wa Wanyama kutoka katika chuo kinachotambuliwa na Baraza.
  2. Awe amemaliza mafunzo ya uanagenzi katika vituo vinavyotambuliwa na Baraza.
  3. Mhitimu aliyesoma nje ya nchi, awe amefaulu mtihani wa Baraza.

KUORODHESHA WATAALAMU WASAIDIZI

  1. Awe na Stashahada ya Tiba na Uzalishaji wa Mifugo kutoka katika chuo kinachotambuliwa na Baraza.

KUANDIKISHA WASAIDIZI WA WATAALAMU WASAIDIZI

  1. Awe na Astashahada ya Tiba na Uzalishaji wa Mifugo kutoka katika chuo kinachotambuliwa na Baraza.
  2. Mhitimu aliyesoma nje ya nchi, awe amefaulu mtihani wa Baraza.

LESENI

Baraza la Veterinari hutoa leseni kwa wataalamu wa kada mbalimbali za taaluma ya mifugo kulingana na vigezo vifuatavyo: -

LESENI KWA WAHIMILISHAJI

Awe na Cheti cha Mafunzo ya Uhimilishaji kutoka kwenye Kituo cha Taifa cha Uhimilishaji.

LESENI ZA WAKAGUZI WA NYAMA

Awe amesajiliwa au kuorodheshwa au kuandikishwa na Baraza.

LESENI KWA WATAALAM WA MAABARA ZA MIFUGO

Awe na Stashahada ya Maabara ya Mifugo kutoka katika chuo kinachotambuliwa na Baraza.

USAJILI WA VITUO VYA HUDUMA ZA MIFUGO

Baraza la Veterinari husajili vituo mbalimbali vya huduma za mifugo kulingana na vigezo vifuatavyo: -

  1. Awe na daktari msimamizi anayetambulika na Baraza
  2. Awe na Mtaalam Msaidizi au Msaidizi wa Mtaalam Msaidizi anayetambulika na Baraza.
  3. Mkataba wa kisheria kati ya mmiliki na wataalam wanaotoa huduma katika kituo husika.
  4. Awe na orodha ya ukaguzi (Inspection Checklist) iliyosainiwa na daktari wa Halmashauri ya Wilaya husika baada ya kukaguliwa.
  5. Uwepo wa vifaa tiba kulingana na aina ya kituo kama atakavyoelekezwa na Daktari wa Mifugo wa Halmashauri ya Wilaya.

UTAMBUZI WA TAASISI ZA MAFUNZO YA MIFUGO

Kifungu cha 5 (2) (d), (e) na (f) (iii) cha Sheria ya Veterinari SURA 319, kinalipa Baraza la Veterinari mamlaka ya kutambua vyuo vinavyotoa mafunzo ya afya ya wanyama, kwa hiyo taasisi au chuo chochote cha mafunzo kinachotaka kutoa mafunzo ya afya ya wanyama lazima kitambuliwe na Baraza.

KUHUISHA USAJILI KWA MADAKTARI WA MIFUGO NA MADAKTARI WABOBEZI WA MIFUGO

Kwa mujibu wa Kifungu cha 23(1) cha Sheria ya Veterinari SURA 319, kila Daktari wa Mifugo au Daktari Mbobezi wa Mifugo aliyesajiliwa atahuisha usajili wake kwa kulipa ada ya kila mwaka.

Ada ya kuhuisha inapaswa kulipwa katika mwaka wa kalenda.

Pale ambapo Daktari wa Mifugo au Daktari Mbobezi wa Mifugo aliyesajiliwa atashindwa kulipa ada ya kuhuisha kila mwaka kabla ya kuisha kwa cheti kilichopo cha usajili, Baraza linaweza kuhuisha usajili iwapo maombi yatafanywa ndani ya miezi sita baada ya kumalizika kwa muda;

Baada ya kipindi hicho cha miezi sita, Daktari wa Mifugo au Daktari Mbobezi wa Mifugo aliyesajiliwa atakuwa hajahuisha usajili wake, Baraza litasimamisha usajili wake kwa mwaka mmoja, na iwapo baada ya mwaka mmoja Daktari wa Mifugo au Daktari Mbobezi wa Mifugo atashindwa kuhuisha usajili, basi Baraza, kwa kuzingatia Kifungu cha 27 cha Sheria ya Veterinari, litafuta usajili na kuondoa jina lake kwenye daftari la usajili.

Kiasi cha ada za kuhuisha kitalipwa kwa mujibu wa Kanuni za Veterinari (Ada na Tozo Nyingine) ya Mwaka, 2015.

KUHUISHA KWA WATAALAMU WA WASAIDIZI NA WASAIDIZI WA WATAALAM WASAIDIZI WA MIFUGO

Kwa mujibu wa Kifungu cha 37(1) cha Sheria ya Veterinari SURA 319, kila Mtaalamu Msaidizi aliyeorodheshwa au aliyeandikshwa atahuisha kwa kulipa ada ya uhuishaji kila mwaka.

Ada ya kuhuisha inapaswa kulipwa katika kalenda ya mwaka; pale ambapo mtu aliyeorodheshwa au aliyeandikishwa atashindwa kulipa kabla ya mwisho wa muda uliopo wa uorodheshaji au uandikishaji, Baraza linaweza kufanya uorodheshaji au uandikishaji huo ikiwa ombi litafanywa ndani ya miezi sita baada ya kumalizika kwa muda.

Iwapo baada ya miezi sita, mtu aliyeandikishwa au kuorodheshwa hajafanya kuhuisha uorodheshwaji au uandikishaji wake, Baraza litasimamisha uorodheshwaji au uandikishwaji kwa muda wa mwaka mmoja na ikiwa baada ya kipindi hicho cha mwaka mmoja Mtaalamu Msaidizi au Msaididi wa Mtaalam Msaidizi atashindwa kuhuisha basi, Baraza, kwa kuzingatia Kifungu cha 34 cha Sheria ya Veterinari, litafuta uorodheshaji au uandikishaji na kuamuru kuondolewa kwa jina la mtu husika katika Orodha au Lisiti ya uandikishaji.

Kiasi cha ada za kuhuisha kitalipwa kwa mujibu wa Kanuni ya Veterinari (Ada na Tozo Nyingine) ya Mwaka, 2015.

KUHUISHA KWA WAHIMILISHAJI

Kwa mujibu wa Kanuni ya 5(1) ya Kanuni za Veterinari (Utoaji Leseni kwa Wahimilishaji) ya Mwaka 2011; kutakuwa na ada ya kuhuisha leseni itakayolipwa kila mwaka na Mhimilishaji aliyeidhinishwa.

Daktari wa mifugo aliyesajiliwa, mtaalamu msaidizi aliyeorodheshwa na msaidizi wa mtaalam msaidizi aliyeandikishwa hawatalipa ada ya uhifadhi kulingana na kanuni ya 5(2) ya Kanuni za Veterinari (Utoaji Leseni kwa Wahimilishaji) ya Mwaka 2011

KUHUISHA KWA WAKAGUZI WA NYAMA

Kwa mujibu wa Kanuni ya 9(1) ya Kanuni za Veterinari (Leseni ya Wakaguzi wa Nyama) ya Mwaka 2011; kutakuwa na ada ya kuhuisha itakayolipwa kila mwaka na mkaguzi wa nyama aliyeidhinishwa.

Daktari wa mifugo aliyesajiliwa, mtaalamu msaidizi aliyeorodheshwa na msaidizi wa mtaalam msaidizi aliyeandikishwa hawatalipa ada ya uhifadhi kulingana na Kanuni ya 9(2) ya Kanuni za Veterinari (Leseni ya Wakaguzi wa Nyama) ya Mwaka 2011.

KUHUISHA KWA WATAALAM WA MAABARA ZA MIFUGO

Kwa mujibu wa Kanuni ya 5(1) ya Kanuni za Veterinari (Leseni ya Wataalamu wa Maabara ya Mifugo) ya Mwaka 2011, kutakuwa na ada ya kuhuisha itakayolipwa kila mwaka kwa Baraza na wataalamu wa maabara ya mifugo walio na leseni.

Ada ya kuhuisha inapaswa kulipwa katika mwaka wa kalenda;

KUHUISHA KWA VITUO VYA HUDUMA YA MIFUGO

Kwa mujibu wa Kanuni ya 34 ya Kanuni za Veterinari (Usajili wa Madaktari wa Mifugo na Vituo vya Huduma za Mifugo) Kanuni za 2004; cheti cha usajili wa kituo cha afya ya wanyama kilichotolewa chini ya kanuni hizi kitakuwa halali mradi tu ada ya mwaka ya kuhuisha imelipwa.

Ada ya kuhuisha vituo vya huduma za mifugo inapaswa kulipwa katika mwaka wa fedha wa serikali.

Kiasi cha ada za uhifadhi na faini ya kuchelewa kuhuisha vitalipwa kulingana na Kanuni ya Veterinari (Ada na Tozo Nyingine) ya Mwaka, 2015.

.