Mkurugenzi Mkuu Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI), Prof. Erick Komba, akimvalisha mbuzi hereni ya kielektroniki ishara ya kuanza kwa Kampeni ya Kitaifa ya Chanjo na Utambuzi wa Mifugo Mkoani Manyara, wakati wa zoezi la Uhamasishaji, Utoaji Chanjo na Utambuzi wa Mifugo katika Kijiji cha Sangaiwe, Julai 3, 2025, Babati - Manyara.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji akioneshwa namna mfumo wa utambuzi wa Mifugo kielektroniki unavyofanya kazi wakati wa ziara yake ya Ukaguzi wa utekelezaji wa zoezi la Kampeni ya kitaifa ya Chanjo na Utambuzi wa Mifugo Wilaya ya Ngorongoro mkoani Arusha Julai 03, 2025. Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa huo Mhe. Kenan Kihongosi.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji akishuhudia namna zoezi la uchanjaji mifugo linavyofanyika wakati wa ukaguzi wa utekelezaji wa zoezi hilo Wilaya ya Ngorongoro mkoani Arusha Julai 03, 2025.
Mkurugenzi wa Huduma za Mifugo nchini Dkt. Benezeth Lutege akitoa chanjo ya ugonjwa wa Sotoka ya Mbuzi na Kondoo wakati wa kuanza kwa kampeni ya kitaifa ya Chanjo na Utambuzi wa Mifugo Wilaya ya Longido mkoani Arusha Julai 02,2025.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akifurahia jambo na Afisa Tehama kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi Bw. Joseph Nkwabi wakati akiangalia namna mfumo wa utambuzi wa Mifugo kupitia hereni za kielektronoki unavyofanya kazi muda mfupi baada ya kuzindua kampeni ya Chanjo na utambuzi wa Mifugo kwenye viwanja vya Nyakabindi, Bariadi mkoani Simiyu Juni 16, 2025.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji akisoma Hotuba ya Bajeti ya Wizara hiyo Bungeni jijini Dodoma Mei 23, 2025.