Habari

  • WAZIRI ULEGA AKUTANA NA WAWEKEZAJI KUTOKA POLAND

    January 18, 2024

    Leo Januari 18, 2024, Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega amekutana na Wawekezaji kutoka Kampuni ya Uwekezaji ya Contractus ya nchini Poland ambao wameonesha nia ya kufanya uwekezaji kwenye tasnia ya Maziwa hapa nchini.

  • ​PWANI IPO TAYARI KUTEKELEZA BBT-LIFE-MCHATTA

    January 15, 2024

    Katibu Tawala Mkoa wa Pwani Bw. Rashid Mchatta amekutana na ujumbe kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi upande wa sekta ya Mifugo Januari 15, 2024 na kufanya nao mazungumzo kuhusu namna ya kutekeleza mradi wa "Jenga kesho iliyo bora kwa wajasiriamali wanawake na Vijana (BBT-LIFE) kwa Mkoani humo.

  • ​​“MAJONGOO BAHARI, MWANI, KAA NI BIASHARA KUBWA”

    January 15, 2024

    Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega amewahimiza wananchi wanaoishi Mtwara na maeneo mengine ya ukanda wa Pwani ya Bahari ya Hindi kuchangamkia fursa ya ufugaji wa Majongoo Bahari, Kaa, Kambakochi pamoja na kufanya kilimo cha Mwani kwa sababu mazao hayo yanahitajika sana katika nchi za Asia hususan China.

  • ​​TANZANIA, RWANDA KUSHIRIKIANA KUKUZA TASNIA YA MAZIWA

    January 13, 2024

    Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega na Waziri wa Kilimo, Maliasili, na Mifugo wa Jamhuri ya Rwanda, Mhe. James Kabarebe wamesaini hati ya makubaliano ya kushirikiana kuendeleza tasnia ya maziwa baina ya nchi hizo mbili.

.