​PWANI IPO TAYARI KUTEKELEZA BBT-LIFE-MCHATTA

Imewekwa: Monday 15, January 2024

PWANI IPO TAYARI KUTEKELEZA BBT-LIFE-MCHATTA

Katibu Tawala Mkoa wa Pwani Bw. Rashid Mchatta amekutana na ujumbe kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi upande wa sekta ya Mifugo Januari 15, 2024 na kufanya nao mazungumzo kuhusu namna ya kutekeleza mradi wa "Jenga kesho iliyo bora kwa wajasiriamali wanawake na Vijana (BBT-LIFE) kwa Mkoani humo.

Akiongoza kikao hicho Bw. Mchatta ameipongeza na kuishukuru Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa kupeleka programu hiyo mkoani kwake ambapo ameahidi kutoa ushirikiano wa kutosha wakati wote wa utekelezaji wake.

"Tunatambua tija kubwa watakayoipata vijana hawa na wanawake watakaofanikiwa kuchaguliwa kuingia kwenye programu hii hivyo niwashukuru sana kwa kuuleta mpango huu hapa Pwani" Amesema Bw. Mchatta.

Akizungumza wakati wa kikao hicho Mkurugenzi msaidizi wa utafiti na Mafunzo kutoka Wizara ya mifugo na Uvuvi (Mifugo) Dkt Hassan Mrutu amesema kuwa utekelezaji huo umewalenga vijana na wanawake katika suala zima la Ufugaji wa kibiashara ambapo jumla ya vijana 30 watakaochaguliwa wanatarajiwa kunufaika na mpango huo utakaotekelezwa kwa siku 90.

Mazungumzo hayo baina ya pande hizo yamefanyika kwenye Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo ambapo mbali na watalaam hao kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi pia yalihudhuriwa na wataalam kutoka Sekretariet ya Mkoa.

.