Habari

  • WACHUNAJI WA NGOZI WATAKIWA KUWA NA LESENI

    December 17, 2020

    Wataalamu wa Mifugo wanaosimamia machinjio nchini wametakiwa kuhakikisha wachunaji wa Ngozi za Wanyama wawe ni wale waliopata mafunzo na wamepewa Leseni ya uchunaji ili ngozi inayochunwa iwe na ubora utakaofaa kuuzwa ndani na nje ya nchi.

  • WIZARA YA MIFUGO NA UVUVI YAANZA KUSAKA VIPAUMBELE VYA BAJETI 2021/22

    December 16, 2020

    Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Pauline Gekul amesema kwa kushirikiana na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki wameanza kufanya kazi kwa kasi kubwa ili kufahamu vipaumbele vya wizara hiyo, ambavyo vinapaswa kujumuishwa katika bunge la bajeti kwa mwaka wa fedha 2021/22.

  • TAARIFA ZA MAGONJWA YA MIFUGO ZAWAGHARIMU WATAALAMU 19 WA AFYA YA WANYAMA

    December 16, 2020

    ​Wataalamu tisa wa afya ya wanyama kutoka halmashauri za wilaya hapa nchini, wamepewa onyo kali kwa kutowasilisha taarifa za magonjwa ya mifugo kwa Idara ya Huduma za Mifugo iliyo chini ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi huku wataalamu 10 wakipewa wiki moja kuwasilisha ushahidi wa wao kuwasilisha taarifa hizo.

  • SERIKALI YAJA NA MKAKATI WA CHANJO ZA MAGONJWA MUHIMU YA MIFUGO KOTE NCHINI

    December 16, 2020

    Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Pauline Gekul ameagiza kuandaliwa kwa mkakati shirikishi wa kupeleka chanjo kwa wafugaji kuanzia mwezi Februari Mwaka 2021 kupitia programu za chanjo ya magonjwa muhimu zitakazosimamiwa na wizara.

.