Habari

  • TALIRI YAJIKITA KUTATUA CHANGAMOTO ZA WAFUGAJI

    February 19, 2021

    Kaimu Mkurugenzi Mkuu, Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI), Dkt. Jonas Kizima amesema utafiti wanaoufanya umejikita katika kutatua changamoto za mbegu bora za mifugo na mbegu bora za malisho kwa wafugaji ili sekta ya mifugo iweze kuchangia vyema katika pato la Taifa.

  • MAWAKALA WA KUKU WASIOTAMBULIKA KUKAMATWA

    February 18, 2021

    Chama cha Wafugaji wa Kuku wa Nyamanchini (TABROFA) kimetakiwa kuwa na ushirikiano ili kutokomeza changamoto wanazozipata wafanyabiashara wa kuku hasa mawakala wasiotambulika wanaouza vifaranga vya kuku wa nyama pamoja na vyakula vya kuku kwa bei ya juu katika maeneo mbalimbali nchini.

  • UHABA WA WATAALAM WENYE UJUZI KILIO KWA WAWEKEZAJI

    February 18, 2021

    Mratibu na Mkurugenzi wa Operesheni, Kiwanda cha Kutengeneza Chanjo cha Hester, Tina Towo Sokoine amesema kuwa lengo la kiwanda hicho ni kutumia Wataalam wa ndani lakini uhaba wa Wataalam wa masuala ya sayansi wenye ujuzi hasa wa vitendo unaelekeakukwamisha dhamira yao hiyo.

  • NARCO YAAGIZWA KUWANYANG'ANYA VITALU WALIOKIUKA MKATABA

    February 18, 2021

    Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba Ndaki ameiagiza Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO) kuwanyang'anya wale wote walioshindwa kuendeleza vitalu walivyokodishwa katika ranchi za kampuni hiyo kwa sababu wamekiuka masharti ya mkataba.

.