Nifanyeje?
- Zipi sifa za kuorodheshwa kama msaidizi wa mtaalam wa mifugo? (Enlisted Paraprofessional Assistant)
- Zipi sifa za kujiandikisha kama mtaalam msaidizi wa mifugo? (Enrolled Paraprofessional).
- Daktari wa mifugo asiye mtanzania (Foreigner) anasajiliwa vipi na Baraza.
- Daktari wa mifugo asiye Mtanzania anaweza kusajiliwa na kufanyakazi hapa nchini? (Temporary and permanent registration)?
WANAWAKE WAHIMIZWA KUJIUNGA KATIKA VIKUNDI

Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Prof. Riziki Shemdoe amewahimiza Wanawake wanaojihusisha na Uvuvi Mdogo wajiunge katika vikundi kwa lengo la kupata fursa ya kukopeshwa vifaa vya kisasa ikiwemo maboti ili wawe na uwezo wa kwenda kuvua samaki katika maji mengi.
Prof. Shemdoe ametoa rai hiyo wakati akifungua warsha ya kujenga uwezo kwa vyama, ushirika na vikundi vya Wanawake wanaojihusisha na Uvuvi Mdogo Barani Afrika unaofanyika jijini Dar es Salaam kuanzia leo Disemba 5 hadi 7, 2023.
Alisema kuwa ili kina mama hao waweze kuondokana na shughuli za kununua samaki katika mialo, wajiunge katika vikundi, watafute manahodha wao ili waingie katika uvuvi na kuepukana na shughuli ya kupara samaki.
Aliongeza kuwa Mhe. Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa shilingi Bilioni 11 kwa ajili ya kukopesha maboti kwa wavuvi hapa nchini, hivyo aliwahimiza wakinamama kuchangamkia fursa hiyo ili waweze kuboresha shughuli zao na uchumi wao kwa ujumla.
Aidha, Prof. Shemdoe alitumia fursa hiyo pia kuwahimiza wakinamama hao kutumia mkutano huo kubadilishana uzoefu na kutengeneza uhusiano wa kibiashara ikiwemo kupeana fursa mbalimbali za kibiashara baina ya maeneo wanayotoka.
Mkutano huo ulioandaliwa na Shirika la Kimataifa la Kilimo na Chakula Duniani (FAO) kwa kushirikiana na Wizara ya Mifugo na Uvuvi umeudhuriwa na Wanawake kutoka nchi zaidi ya ishirini (20) za Bara la Afrika na Bara la