Nifanyeje?
- Zipi sifa za kuorodheshwa kama msaidizi wa mtaalam wa mifugo? (Enlisted Paraprofessional Assistant)
- Zipi sifa za kujiandikisha kama mtaalam msaidizi wa mifugo? (Enrolled Paraprofessional).
- Daktari wa mifugo asiye mtanzania (Foreigner) anasajiliwa vipi na Baraza.
- Daktari wa mifugo asiye Mtanzania anaweza kusajiliwa na kufanyakazi hapa nchini? (Temporary and permanent registration)?
WAFUGAJI WAHAMASISHWA KULIMA MALISHO

WAFUGAJI WAHAMASISHWA KULIMA MALISHO
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega ameendelea kuwahimiza wafugaji kuhakikisha wanatenga maeneo kwa ajili ya kulima malisho ili kuwa na uhakika wa malisho kwa ajili ya mifugo yao wakati wote.
Waziri Ulega ametoa wito huo alipotembelea shamba la mbegu na malisho la wizara hiyo lililopo Vikuge, Wilayani Kibaha, Mkoani Pwani, Disemba 13, 2023. Shamba hilo ni miongoni mwa mashamba ya malisho ya mifugo ambayo Serikali imefanya uwekezaji mkubwa.
Wakati akikabidhi mbegu za malisho za aina ya Juncao kwa baadhi ya wafugaji waliofika shambani hapo ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha wafugaji kuona umuhimu wa kulima malisho, Waziri Ulega alisema kuwa kila mfugaji ni muhimu awe na eneo la malisho kwani itawasaidia kuondokana na migogoro baina yao na wakulima.
"Kwa wafugaji waliokuwa wanauliza wapi watapata mbegu bora sasa zinapatikana kwa wingi hapa Vikuge kilo 1 itakuwa ikiuzwa Shilingi 4,000.Lakini kwa siku za usoni Serikali itaangalia namna ya kupunguza hii bei,"amesema Waziri Ulega.
Mheshimiwa Ulega amesema katika shamba hilo kuna tani 78 za mbegu za majani aina ya Juncao ambayo ni bora kwa ajili ya kuzalisha malisho ya mifugo.Amewataka wafugaji kupanda mbegu hizo ili kuondokana na changamoto ya kuvamia mashamba ya wakulima.
"Shime, nasisitiza tena, wafugaji karibuni sana kununua mbegu hizi, tukapande ili tuweze kupunguza jambo la mifugo kufa kwa sababu ya kukosa malisho au mifugo kwenda kuvamia mashamba ya wakulima, ni aibu kubwa sana kuona mkulima na mfugaji wanagombana, tutafute suluhu, na suluhu ya kwanza ni kuwa na malisho ya uhakika", alisema
Naye, Mkurugenzi wa Uendelezaji wa Malisho na Rasilimali za Vyakula vya Mifugo, Dkt. Asimwe Rwiguza amesema kuwa mbegu hizo za Juncao zilizopo katika shamba la Vikuge litasaidia kupunguza changamoto ya malisho huku akisema kuwa mpango wa Wizara ni kusambaza mbegu za malisho hayo katika mashamba mengine ya Wizara yaliyopo mikoani ili kusogeza huduma hiyo karibu na wananchi.