WADAU WA TASNIA YA NDEGE WAFUGWAO WAIPONGEZA SERIKALI KWA KUTATUA KERO ZAO

Imewekwa: Monday 22, June 2020

Wadau wa tasnia ndogo ya ndege wanaofugwa wameipongeza Serikali kwa kutatua kero za kisera ambazo zilikuwa zikidumaza tasnia hiyo.

Hayo yamesemwa na Katibu wa chama Kikuu cha Wadau wa Tasnia ya Kuku (PAT), Manase Mrindwa katika kikao cha Wadau wa tasnia ya kuku kilichofanyika jijini Dodoma Juni 18,2020.

Akiongea kwenye kikao hicho Mrindwa alisema kuwa bajeti ya Serikali ya mwaka 2020/2021 imetoa majibu kwa kero zao kwa kuondoa kodi kwenye mayai ya kutotolesha vifaranga yanayotoka nje ya nchi, imepunguza tozo kwenye vyakula vya mifugo vinavyosafirishwa nje ya nchi na kupunguza tozo kwenye mayai yanayosafirishwa nje ya nchi.

“Unafuu huu wa tozo tunategemea utaiinua tasnia hii ya ndege wanaofugwa hapa Tanzania, alisema Mrindwa.

Pamoja na pongezi hizo Mrindwa alieleza changamoto zilizowakumba kufuatia mlipuko wa maradhi ya Korona ambazo zimechangia kupungua kwa ulaji wa bidhaa za kuku kutokana na mdororo wa biashara uliopelekea kufungwa kwa baadhi ya shughuli za biashara ikiwemo mahoteli, migahawa, vyuo, shule na kusitishwa kwa shughuli zinazoleta mikusanyiko ya watu.

"Kudumaa kwa biashara zinazohitaji mazao ya kuku, kupungua kufuga kuliathiri viwanda vinavyozalisha vyakula vya mifugo, uingizaji wa bidhaa za kuku kutoka nje zilisitishwa, wafugaji waliokopa kwenye taasisi mbalimbali za kifedha walipata shida katika marejesho." Aliongeza Mrindwa

Aidha, Mrindwa alisema kuwa kufuatia kupungua kwa changamoto ya mlipuko wa maradhi ya Korona shughuli za kibiashara zimeanza kurejea katika hali yake jambo ambalo litasaidia kuimarisha biashara hiyo huku akitaja shughuli ambazo zimeshaanza kurejea kama vile usafiri wa anga, utalii, uzalishaji katika viwanda, mashamba ya kuku wazazi ambayo yameanza kupokea vifaranga vya kuku na kuanza kuingia nchini virutubisho vya kutengenezea vyakula vya mifugo.

Aliongeza kuwa kwa sasa wafugaji wameanza kuongeza na kuimarisha shughuli zao za ufugaji hivyo kupelekea kuwa na changamoto ya ongezeko la mahitaji ya vifaranga wa nyama na wa mayai.

"Serikali iendelee kujadiliana na nchi jirani hususani Kenya na Zambia ili shughuli za mipakani ziweze kufanyika kama awali na usumbufu wa madereva na ucheleweshwaji wa mizigo uishe ili kurahisisha upatikanaji wa bidhaa za mifugo ili biashara iweze kuimarika zaidi, alisisitiza Mrindwa.

Katika hatua nyingine, Wadau hao wamekiri kujifunza namna ya kuweka mkakati wa kuimairisha ulaji wa nyama ya kuku na mayai hapa nchini, kuhamasisha uanzishwaji wa viwanda vya kutengeneza dawa za kuku na uwekezaji katika maghala na kuiomba serikali kuendelea na mchakato wa kuzalisha soya ya kutosha kwa mahitaji ya vyakula vya mifugo.

"Hivi sasa kwa wastani Mtanzania mmoja anakula mayai 75 kwa mwaka wakati kiwango cha FAO ni kula mayai 200 kwa mwaka, pia Mtanzania anakula kilo 15 za nyama kwa mwaka wakati FAO inapendekeza kula kilo 45 kwa mwaka." Alifafanua Mrindwa.

.