Nifanyeje?
- Zipi sifa za kuorodheshwa kama msaidizi wa mtaalam wa mifugo? (Enlisted Paraprofessional Assistant)
- Zipi sifa za kujiandikisha kama mtaalam msaidizi wa mifugo? (Enrolled Paraprofessional).
- Daktari wa mifugo asiye mtanzania (Foreigner) anasajiliwa vipi na Baraza.
- Daktari wa mifugo asiye Mtanzania anaweza kusajiliwa na kufanyakazi hapa nchini? (Temporary and permanent registration)?
VIJANA WALIOITIKIA WITO WA MHE. RAIS KUWEZESHWA

VIJANA WALIOITIKIA WITO WA MHE. RAIS KUWEZESHWA ZAIDI
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega amemuelekeza Naibu Katibu Mkuu, Sekta ya Mifugo, Prof. Daniel Mushi kuhakikisha anawawezesha vijana wa kikundi cha Kanani Msomera walionzisha wao wenyewe programu yao ya BBT kwa lengo la kujikwamua kiuchumi lakini pia kuunga mkono nia na dhamira njema ya Mhe. Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuinua vijana kiuchumi kupitia programu ya Jenga Kesho Iliyobora (BBT).
Waziri Ulega ametoa maelekezo hayo Machi 7, 2024 wakati wa ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo ya sekta ya mifugo inayotekelezwa katika Kijiji cha Msomera kilichopo wilayani Handeni, mkoani Tanga ambapo aliwatembelea vijana hao ambao wameanzisha programu yao ya kunenepesha mifugo na kuiuza.
“Nyinyi hamkutaka kusubiri, mmeona programu ya Mhe, Rais Samia ya BBT na mkasema hapa Msomera mnaanzisha BBT yenu, hongereni sana, sasa natoa maelekezo kwa Naibu Katibu Mkuu kuwaangalia kwa ukaribu vijana hawa walioanzisha BBT wao wenyewe kuhakikisha wanapewa kipaumbele katika elimu ya ufugaji na mitaji kwa kuwaunganisha na Benki ya Maendeleo ya Kilimo(TADB) ili wapatiwe mikopo nafuu isiyokuwa na riba”, alisema
Waziri Ulega amesema kwa sababu hao vijana wamejiunga juhudi za Mhe. Rais kwa vitendo bila kusubiri ni lazima waungwe mkono na hapo hapo aliwakabidhi Mbegu za Malisho na Mbuzi (10) waliotolewa na Shirika la Heifer International kama ruzuku ikiwa ni sehemu ya kuwatia chachu katika jitihada zao hizo.
Naye, Mkurugenzi Mtendaji, Heifer International, Bw. Mark Tsoxo amesema kuwa wao tayari wameshirikiana na kikundi hicho cha vijana na wameshawapatia elimu juu ya biashara, masoko na uendeshaji wa vikundi, huku pia wakiwapatia mbuzi vijana hao ambao wameona ndoto ya Mhe, Rais ya kuwainua vijana kupitia program ya BBT.