Nifanyeje?
- Zipi sifa za kuorodheshwa kama msaidizi wa mtaalam wa mifugo? (Enlisted Paraprofessional Assistant)
- Zipi sifa za kujiandikisha kama mtaalam msaidizi wa mifugo? (Enrolled Paraprofessional).
- Daktari wa mifugo asiye mtanzania (Foreigner) anasajiliwa vipi na Baraza.
- Daktari wa mifugo asiye Mtanzania anaweza kusajiliwa na kufanyakazi hapa nchini? (Temporary and permanent registration)?
ULEGA: TANGAZENI VITALU KWA AJILI YA UWEKEZAJI

ULEGA: TANGAZENI VITALU KWA AJILI YA UWEKEZAJI
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega amewaagiza Naibu Katibu Mkuu, Sekta ya Mifugo, Prof. Daniel Mushi na Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera kuhakikisha kuwa maeneo yote yaliyopo katika Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO) mkoani Kagera ambayo hayana mgogoro yatangazwe kwa ajili ya uwekezaji.
Ulega ametoa maelekezo hayo wakati wa kikao chake na Viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Kagera kilichofanyika leo Januari 22, 2024 chenye lengo la kumaliza migogoro iliyopo baina ya wananchi na Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO).
Amesema maeneo ambayo yameshapimwa na ambayo hayana mgogoro yatangazwe ili wawekezaji wenye uwezo waweze kupewa kwa ajili ya kufanya ufugaji wenye tija.
Sambamba na hayo amewataka Wataalamu kurejea upya kwenye maeneo yote ambayo yameonekana yana migogoro ili kutatua changamoto zilizopo na kuwezesha maeneo hayo yaweze kuendelezwa na wawekezaji wenye uwezo.