Nifanyeje?
- Zipi sifa za kuorodheshwa kama msaidizi wa mtaalam wa mifugo? (Enlisted Paraprofessional Assistant)
- Zipi sifa za kujiandikisha kama mtaalam msaidizi wa mifugo? (Enrolled Paraprofessional).
- Daktari wa mifugo asiye mtanzania (Foreigner) anasajiliwa vipi na Baraza.
- Daktari wa mifugo asiye Mtanzania anaweza kusajiliwa na kufanyakazi hapa nchini? (Temporary and permanent registration)?
ULEGA: RAIS SAMIA ANATAKA UFUGAJI WA KISASA

ULEGA: RAIS SAMIA ANATAKA UFUGAJI WA KISASA
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega amesema kuwa dhamira ya Mhe. Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kuona wafugaji wanafuga kisasa na ndio maana amewapelekea mbegu za malisho ili wafugaji waondokane na changamoto ya malisho hapa nchini.
Waziri Ulega ameyasema hayo alipokuwa akikabidhi mbegu za malisho kwa wafugaji wa kijiji cha Msomera wakati wa ziara yake ya siku moja ya kukagua maendeleo ya utekelezaji wa miradi ya sekta ya mifugo katika kijiji hicho kilichopo wilayani Handeni, mkoani Tanga Machi 7, 2024.
“Na haya ni maelekezo ya Mhe. Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kwamba anataka kuona ufugaji wa kisasa, kwa hivyo kazi kwenu wafugaji, amekupeni mbegu hizi zenye thamani kubwa ili muweze kupanda na nikija hapa tena baada ya mvua nikute mashamba ya malisho yameenea”, alisema
Aidha, Ulega amewataka wafugaji hao watakapo panda na kuvuna malisho yao kuhakikisha wanaweka akiba ili yaweze kuwafaa wakati wa kiangazi.
Naye Mwenyekiti wa Chama cha Wafugaji Tanzania, (CWT), Bw. Murida Mushota amewataka wafugaji kutumia mbegu hizo kuleta mabadiliko kwenye sekta ya mifugo.