ULEGA AZINDUA MPANGO WA TAIFA WA KUHIFADHI KASA BAHARINI

Imewekwa: Sunday 31, March 2024

ULEGA AZINDUA MPANGO WA TAIFA WA KUHIFADHI KASA BAHARINI

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega amesema Mpango wa Taifa wa Miaka 5 wa Kuhifadhi Kasa wa Baharini ambao ameuzindua mapema leo ukitekelezwa ipasavyo utasaidia kuwalinda Kasa hao ambao wapo hatarini kutoweka.

Waziri Ulega ameyasema hayo Wilayani Mkuranga, Mkoani Pwani Machi 28, 2024 wakati akizindua Mpango huo wa Taifa wa Miaka 5 wa Kuhifadhi Kasa wa Bagarini unaotekelezwa na Shirika la Sea Sense chini ya ufadhili wa Shirika la USAID.

“Sheria ya Uvuvi Sura namba 279, Sheria ya Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu namba 146 na kanuni za uvuvi za mwaka 2009 zimeainisha kuwa kasa wa baharini wapo katika hatari ya kutoweka na hivyo wanahitaji usimamizi na ulinzi mahususi”, alisema

.