ULEGA AWATAKA MAAFISA UGANI KUWA WABUNIFU KUSAIDIA WAFUGAJI

Imewekwa: Monday 18, March 2024

ULEGA AWATAKA MAAFISA UGANI KUWA WABUNIFU KUSAIDIA WAFUGAJI

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega amewataka maafisa ugani wa mifugo kote nchini kuwa wabunifu na kuweka mikakati ya kudumu kuhakikisha katika maeneo wanayofanyia kazi wanawasaidia wafugaji kuzalisha malisho kwa ajili ya mifugo yao.

Waziri Ulega ametoa maelekezo hayo wakati akifungua mafunzo rejea ya maafisa ugani 1000 wa nchi nzima yaliofanyika mjini Kibaha mkoani Pwani Machi 18, 2024.

“Hili jambo la malisho ni lazima mkalitekeleze kwa vitendo katika maeneo yenu ili tubadilishe mtazamo na fikra za wafugaji wetu wa kuhamahama kutafuta malisho, jambo hili linawezekana kwa kuwa na mikakati ya pamoja”, alisema

.