ULEGA AWAKARIBISHA WASAUDIA KUWEKEZA SEKTA YA MIFUGO, UVUVI

Imewekwa: Wednesday 15, November 2023

ULEGA AWAKARIBISHA WASAUDIA KUWEKEZA SEKTA YA MIFUGO, UVUVI Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega amewakaribisha wafanyabiashara na Wawekezaji wa nchini Saudia Arabia kuja kuwekeza nchini kwa sababu kuna mazingira mazuri ya uwekezaji yaliyowekwa na Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan. Waziri Ulega alitoa wito huo katika Mkutano wa kujadili masuala ya uwekezaji baina ya Tanzania na Saudi Arabia uliofanyika jijini Riyadh, nchini Saudi Arabia Novemba 11, 2023. Waziri Ulega alieleza katika mkutano huo kwamba Tanzania ina fursa nyingi za uwekezaji katika sekta za kilimo, mifugo, uvuvi, madini, ujenzi na utalii. "Tanzania ipo tayari kufanya biashara na Wawekezaji wa Saudi Arabia, milango iko wazi Tanzania ina mazingira mazuri ya biashara, kiuchumi na kisiasa, rasilimali za kutosha, soko zuri la bidhaa kutokana na jiogragia yake na zaidi ya yote Serikali inasaidia Wawekezaji kufikia malengo yao kupitia Kituo cha chetu cha Uwekezaji Tanzania

.