ULEGA ATEMBELEA TANCHOICE

Imewekwa: Thursday 14, December 2023

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega akiongeza na Uongozi wa Machinjio ya kisasa ya TANCHOICE alipotembelea Machinjio hayo yaliyopo Wilayani Kibaha, Mkoani Pwani Disemba 13, 2023, ambapo aliwapongezi kwa kazi nzuri wanayoifanya ya kuchagiza biashara ya nyama nje ya nchi.

Alisema mkakati wa Serikali kupitia Wizara yake ni kufungua soko la china ili nyama ya Tanzania iweze kuuzwa huko huku akiwasisitiza kuona namna bora ya wao kumuunga mkono Mhe. Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kupitia programu yake ya kielelezo ya Jenga Kesho Iliyobora( BBT-LIFE).

.