ULEGA ASHIRIKI MKUTANO WA WIZARA ZA KISEKTA NA AFDB

Imewekwa: Monday 04, December 2023

ULEGA ASHIRIKI MKUTANO WA WIZARA ZA KISEKTA NA AFDB

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega ameshiriki Mkutano wa Wadau, Viongozi na Wizara za kisekta na AFDB wa pamoja wa upili (Bilateral Meeting) kujadili mpango wa upatikanaji wa fedha za Mradi wa ujenzi wa Bwawa la Songwe kwa kushirikiana kati ya Tanzania na Malawi.

Lengo la mkutano huo ni kufanikisha kukabiliana na Mabadiliko ya TabiaNchi kuzuia mafuriko, upatikanaji wa maji, kuzalisha umeme, kutumika kwa kilimo cha umwagiliaji, na matumizi ya shughuli za Uvuvi na kunyweshea Mifugo.

Mkutano huo ulioandaliwa na Wizara ya Maji ya Maji Tanzania na Wizara ya Maji na Usafi wa Mazingira Malawi kwa pamoja umeudhuriwa pia na Mawaziri wa Kisekta kwa upande wa Tanzania ikiwa ni pamoja na Waziri wa Fedha Mhe Mwigulu Nchemba, Waziri wa Kilimo Mhe Hussein Bashe, Waziri wa Kilimo, Zanzibar, Mhe Shamata Khamisi wakiambatana na Makatibu wakuu wa Wizara hizo.

Mkutano huo umeongozwa na Mwenyekiti wa SongweCom, Waziri wa Maji Tanzania, Mhe. Jumaa Aweso akishirikiana na Mwenyekiti Mwenza Waziri wa Maji Malawi, Mhe. Abida Sidik Mia.

Mkutano huo umefanyika leo Disemba 3, 2023 kando ya Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabia Nchi (COP 28) unaoendelea katika mji wa Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu ambapo Mhe. Ulega anahudhuria.

.