Nifanyeje?
- Zipi sifa za kuorodheshwa kama msaidizi wa mtaalam wa mifugo? (Enlisted Paraprofessional Assistant)
- Zipi sifa za kujiandikisha kama mtaalam msaidizi wa mifugo? (Enrolled Paraprofessional).
- Daktari wa mifugo asiye mtanzania (Foreigner) anasajiliwa vipi na Baraza.
- Daktari wa mifugo asiye Mtanzania anaweza kusajiliwa na kufanyakazi hapa nchini? (Temporary and permanent registration)?
TUMEANDAA MPANGO WA MAGEUZI YA SEKTA YA MIFUGO NCHINI-BITEKO111
.jpg)
TUMEANDAA MPANGO WA MAGEUZI YA SEKTA YA MIFUGO NCHINI-BITEKO
◼️ Aagiza Wizara ya Mifugo kuendelea kutoa elimu ya ufugaji wa kibiashara
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema kuwa Serikali imeandaa mpango wa mageuzi ya sekta ya mifugo ambao utasaidia kupata ufumbuzi wa changamoto zinazoikabili sekta ya mifugo nchini.
Dkt. Biteko ameyasema hayo leo Juni 16, 2024 Kibaha, Pwani wakati akifunga Maonesho na Mnada wa Mifugo kwa mwaka 2024.
“ Wizara msichoke wala msiache kuwapa elimu wafugaji wetu, lazima tukubali kuwa wamekuwa hivyo kwa miaka mingi mabadiliko lazima yatokee na lazima tujue kuwa maeneo mengi yanayohitaji ardhi yanaongezeka ikiwa ni pamoja na mifugo lakini ardhi haiongezeki. Hivyo, tuendelee kuwapa elimu ya ufugaji wa kisasa na kuwahimiza wafugaji waje kwenye maonesho kama haya ili wapate ujuzi na teknolojia itakayowasaidia”, amesema Dkt. Biteko.
Aidha Dkt. Biteko amewataka Wafugaji kuendana na mabadiliko ya Teknolojia na Uchumi yanayoendelea Ulimwenguni kabla hayajawalazimisha kubadilika na kuathiri shughuli zao za ufugaji.
“ Wafugaji msijione dhaifu wala wanyonge unaweza kukuta mfugaji ana ng’ombe 1,000 huyo huwezi kumuita masikini, ng’ombe hao wanaweza kuwa mtaji kinachohitajika ni namna gani unaweza kubadilisha maisha yako kwa kutumia hao ng’ombe ulionao.” Ameongeza Dkt. Biteko.
Katika hatua nyingine, Dkt. Biteko amesema kuwa ni vyema maonesho hayo ya mifugo yakafanyika kikanda ili yaweze kuwafikia wakulima wengi zaidi nchini ikiwa ni pamoja na kuwasaidia kupata ufumbuzi wa changamoto zinazowakabili ikiwa ni pamoja na mbegu bora za mifugo na teknolojia za kisasa za ufugaji.
Naye, Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Alexander Mnyeti amewapongeza washiriki na wadhamini wa maonesho hayo ya mifugo ambayo yanalenga kutoa elimu kwa wafugaji ili kuleta tija.
“Maonesho haya ni ya muhimu na kwa mwaka huu tumeyawekea nguvu zaidi kwa kuwa yanaleta matokeo makubwa na kwa kuwa yamekuwa maelekezo ya viongozi wetu wa Serikali kuwa wafugaji wetu wasifuge kizamani. Lazima sasa ifike mahali wafugaji wetu waondokane na ufugaji wa kizamani kwa mwamvuli wa kimila, ”Amesema Mhe. Mnyeti.
Aidha Mnyeti amewataka wafugaji nchini kuwatumia wataalamu wa mifugo ili waweze kupewa elimu ya ufugaji wa kisasa na wenye tija ili kubadilisha sekta ya mifugo nchini.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafugaji Kibiashara Tanzania, Bw. Naweed Mulla amesema kuwa Jumuiya hiyo inalenga kuwakutanisha pamoja wafugaji, kupeana ushauri na kusaidiana kwenye changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuisaidia Serikali iweze kuwafikia kirahisi wakati wote.
Maonesho na Mnada wa Mifugo kwa mwaka 2024 yaliyofanyika kwa siku tatu ambapo yalizinduliwa na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Alexander Mnyeti Juni 14, 2024.a