Nifanyeje?
- Zipi sifa za kuorodheshwa kama msaidizi wa mtaalam wa mifugo? (Enlisted Paraprofessional Assistant)
- Zipi sifa za kujiandikisha kama mtaalam msaidizi wa mifugo? (Enrolled Paraprofessional).
- Daktari wa mifugo asiye mtanzania (Foreigner) anasajiliwa vipi na Baraza.
- Daktari wa mifugo asiye Mtanzania anaweza kusajiliwa na kufanyakazi hapa nchini? (Temporary and permanent registration)?
SERIKALI kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi imewahakikishia wafugaji kuwa hakuna mifugo itakayopotea.

SERIKALI nchini kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi imewahakikishia wafugaji kuwa hakuna mifugo itakayopotea kutokana na magonjwa mbalimbali.
Haya yameelezwa na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega wakati akizungumza na wafugaji wa Wilaya ya Kibaha Mkoani Pwani, wakati wa ziara ya kikazi ya siku moja alioifanya Mkoani humo kwa lengo la kukagua miradi iliyoko chini ya wizara hiyo.
Amesema Serikali ilibinafsisha Sekta hiyo kwa watu binafsi, lakini kwa sasa imerejeshwa serikalini ili kuwasaidia wafugaji wa aina zote. "Kwa sasa tunazalisha chanjo ya mdondo zaidi ya milioni 100 kwa mwaka, lengo ni kuwafanya wafugaji wa kuku na hasa akinamama waweze kuondokana na umasikini,"amesema Ulega.
Ameongeza madhumuni ya Serikali ya Awamu ya tano ni kuhakikisha nchi inakuwa na mifugo mizuri yenye kuleta tija kwa wafugaji na wawekezaji wa nyama, hivyo amewataka wafugaji kuamini serikali kwa jinsi inavyowapambania katika kuhakikisha soko la bidhaa hiyo inakuwa kubwa na yenye tija kwao.
Aidha ameongeza kuwa kipindi hiki wafugaji nchini wamekuwa wakinyanyaswa na wafanya biashara kwa kuuza chanjo hizo kwa bei ya Sh.35,000 mpaka Sh. 45,000 kutokana na hali hiyo Serikali imeamua kusambaza dawa hizo za chanjo kwa bei ya Sh.20,000, hivyo itawasaidia watanzania wengi na kuondoa vifo vya mifugo.
Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa Wakala maabara ya vetenari Tanzania, Dkt. Furaha Mramba amesema chanjo zinazozalishwa katika maabara hiyo zinaubora uliothibitishwa na mamlaka za maabara za Mifugo Afrika na itakapokamilika itatosheleza mahitaji ya ndani na nyingine kuuzwa nje ya nchini.
Katika ziara hiyo Mhe. Ulega pia ametembelea shamba la kuzalisha malisho ya mifugo lililopo Vikuge Wilayani Kibaha, pamoja Halmashuri ya Chalinze wilayani Bagamoyo kisha kuhutubia mkutano wa hadhara katika kata ya Pangani na kuwaomba wakazi wa kata hiyo kuacha tabia ya kuvamia maeneo yaliotengwa na Serikali kwa ajili ya miradi mbalimbali ya Maendeleo.