Nifanyeje?
- Zipi sifa za kuorodheshwa kama msaidizi wa mtaalam wa mifugo? (Enlisted Paraprofessional Assistant)
- Zipi sifa za kujiandikisha kama mtaalam msaidizi wa mifugo? (Enrolled Paraprofessional).
- Daktari wa mifugo asiye mtanzania (Foreigner) anasajiliwa vipi na Baraza.
- Daktari wa mifugo asiye Mtanzania anaweza kusajiliwa na kufanyakazi hapa nchini? (Temporary and permanent registration)?
SERIKALI KUENDELEA KUWEZESHA UFUGAJI WA KISASA

Na Hamisi Hussein - WMUV, Mwanza.
⬛️ Mhe. Mnyeti akikabidhi Mitamba 10 ya Maziwa kwa UWAMATA
Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi itaendelea kuwezesha ufugaji wa kisasa ili kuongeza tija katika uzalishaji na kukuza uchumi wa wafugaji nchini.
Hayo yameelezwa leo Aprili 19, 2025 na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Alaxender Mnyeti wakati wa kukabidhi ng'ombe 10 wa Maziwa kwa kikundi cha Umoja wa Mapadri Tanzania (UWAMATA) hafla iliyofanyika katika Shamba la Uzalishaji Mifugo lililopo Misungwi mkoani Mwanza.
Mhe. Mnyeti amesema lengo la serikali nikuona inawezesha ufugaji wa kisasa kwa kuhimiza wafugaji kuwa na mifugo michache yenye tija itakayotoa mazao bora yanayokidhi ushindani wa masoko.
" Mhe. Rais wetu anataka kuona ufugaji wa Kisasa unakuwa na tija kwa wafugaji na sisi Wizara tunaendelea kuhimiza ufugaji wa kisasa ambapo tumekuwa tukihamasisha ulimaji wa malisho ambayo yametajwa na wataalam wetu kuwa yanaprotini nyingi" alisema Mhe. Mnyeti.
Kuhusu ng'ombe wa maziwa (Mitamba) waliotolewa na serikali kwa Kikundi cha Umoja wa Mapadri Tanzania (UWAMATA) Mhe. Naibu Waziri Mnyeti amesema zoezi la upandikizaji wa ng'ombe hao limefanywa na Wataalam wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi ili kuwa na uhakika wa uzalishaji wa ng'ombe hao.
Kwa Upande wake Mwenyekiti wa Umoja wa Mapadri Tanzania (UWAMATA) Padri George Nzungu ameishukuru serikali kwa kuwapatia ng'ombe hao kwani wataleta tija ya uzalishaji wa maziwa na kuahidi kuwa balozi wa ufugaji wa kisasa kwa wananchi wanaozunguka eneo lao.
Aidha Mkurugenzi Msaidi wa Idara ya Uzalishaji na Masoko Dkt . Yeremia Sanka amesema ng'ombe hao waliopatikana kutokana na upandikizaji wa mbegu za madume halisi ya maziwa (Friesian) na majike ya kienyeji aina ya Boran na watazalisha kati ya lita 8 hadi 12 kwa siku tofauti na ng'ombe wa asili ambaye anatoa maziwa lita 1.5 hadi 3 tu kwa siku.