Nifanyeje?
- Zipi sifa za kuorodheshwa kama msaidizi wa mtaalam wa mifugo? (Enlisted Paraprofessional Assistant)
- Zipi sifa za kujiandikisha kama mtaalam msaidizi wa mifugo? (Enrolled Paraprofessional).
- Daktari wa mifugo asiye mtanzania (Foreigner) anasajiliwa vipi na Baraza.
- Daktari wa mifugo asiye Mtanzania anaweza kusajiliwa na kufanyakazi hapa nchini? (Temporary and permanent registration)?
PROF. SHEMDOE ATOA MAELEKEZO KWA WAZABUNI WATAKAO SAMBAZA CHANJO NCHINI

PROF. SHEMDOE ATOA MAELEKEZO KWA WAZABUNI WATAKAO SAMBAZA CHANJO NCHINI
Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof. Riziki Shemdoe amewataka wazabuni waliopewa jukumu la kusambaza chanjo kwa ajili ya kampeni ya chanjo ya mifugo nchini kuhakikisha kazi hiyo wanaifanya vyema kwa kushirikiana na wazalishaji.
Ameyasema hayo wakati wa Hafla Fupi ya Utiaji Saini Mikataba baina ya Wizara na Wazabuni hao watakaosambaza Chanjo ya Mifugo Nchini iliyofanyika jijini Dodoma Januari 21, 2025.
Prof. Shemdoe ameongeza kuwa utoaji wa chanjo hiyo kwa mifugo inatakaiwa kufanyika chini ya uangalizi wa wazalishaji kwa kushirikiana na wataalamu watakao kuwa wanafanya kazi hiyo ili kusaidia kutatua changamoto zitakazojitokeza wakati wa zoezi hilo.
Aidha Prof. Shemdoe ametoa shukrani kwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuridhia na kuwezesha utowaji wa chanjo hiyo mwaka huu na kuwapa kipaumbele makampuni yanayozalisha chanjo ndani ya nchi kuweza kusambaza chanjo hiyo nchi nzima.
Kampuni zitakazotumika katika uzalishaji wa chanjo wa chanjo hiyo ni pamoja na Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA), Hester Biosciences Afica Limited (HBAL) na Novel Vaccine and Biological Limited (NOVABI).