NCHI 30 ZAKUTANA DSM KUMJADILI KASA

Imewekwa: Thursday 04, July 2024

NCHI 30 ZAKUTANA DSM KUMJADILI KASA

Wadau kutoka nchi mbalimbali takriban 30 zilizo kando ya Bahari ya Hindi ambazo zimesaini makubaliano ya uhifadhi wa Kasa wa baharini wamekutana kujadili na kupima hatua waliyofikia ya kuwalinda kasa hao tangu wasaini makubaliano.

Hayo yamefahamika wakati Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Prof. Riziki Shemdoe alipokuwa akifungua mkutano wa 9 wa nchi zilizoingia makubaliano ya kulinda Kasa na mazingira yake uliofanyika jijini Dar es Salaam Juni 24, 2024.

Akiongea muda mfupi kando ya mkutano huo, Prof. Shemdoe amesema wadau kutoka nchi hizo 30 wamekutana kuona wamefika wapi tangu waliposaini makubaliano ya kuwalinda Kasa ambao wapo kwenye hatari ya kutoweka duniani.

Katika mkutano huo ambao unafanyika kwa siku nne kuanzia leo Juni 24 hadi 28, 2024, Tanzania ndio mwenyeji kupitia Kitengo cha Uhifadhi wa Bahari na Maeneo Tengefu (MPRU) kilichopo chini ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi.

.