Naibu Waziri Mhe. Abdallah Ulega akikabidhi vifaranga kwa kikundi cha ufugaji bora Dodoma

Imewekwa: Wednesday 29, August 2018

YALIYOJIRI KATIKA ZOEZI LA UGAWAJI WA VIFARANGA KUTOKA KWA AKM GLITTERS CO. KTD KWA KIKUNDI CHA UFUGAJI BORA WA KUKU DODOMA (CHAWAKUBODO) ILIYOFANYIKA KATIKA VIWANJA VYA NYERERE SQUARE.

Mgeni rasmi katika kuendesha zoezi la ugawaji wa vifaranga alikuwa Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega akiwa na Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Mizengo Peter Pinda pamoja na Mkuu wa Wilaya wa Dodoma Mhe. Patrobas Katambi.

#Nawapongezeni kwasababu tupo katika utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi wa Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2015-2020 ambayo inaelekeza Vyama Vya Ushirika vya Wafugaji alisema, - Mhe. Ulega.

#Mkakati wetu kama Serikali kupitia Wizara yetu ni kuhakikisha tunawasaidia Watanzania katika ufugaji wa kuku, ng'ombe na samaki kwa kushirikiana kwa pamoja na kujiimarisha vizuri, kuna msemo usemao " Umoja ni nguvu Utengano ni udhaifu", alisema - Mhe. Ulega

#Pamoja na mkakati wa kuhakikisha vyama vya ushirika vinapata nguvu kupitia Wizara yetu, tunafahamu kuku ni jambo la kuitajika Nchini lakini ulaji wa kuku unaonekana ni anasa - Mhe. Ulega

#Ambapo ilitakiwa kuku iwe ni bidhaa ambayo inapatikana kirahisi zaidi kuliko nyama nyingine, nataka niwahakikishie sisi tunaenda kupafikia huko na Wizara yangu kwa pamoja tunaunga mkono Ushirika na tunataka wafugaji wetu wasonge mbele ambapo tunakwenda na zoezi kubwa la kufuga kuku kibiashara. - Mhe. Naibu Waziri

#Vilevile kwa mwaka asilimia zaidi ya 50 ya kuku wanaofugwa kwa mjini na vijiji wanakufa kutokana na maradhi mabaya ya mdodo au kideri ambapo magonjwa yanaangamiza kuku wengi sana hapa Nchini. - Mhe. Ulega.

#Awali ya yote tumejipanga vyema kuanzia mwezi wa 9 mwaka huu tunaanza zoezi la kupiga chanjo mifugo yetu na zoezi hili la kuchanja mifugo ni la lazima, kwa upande wa kuku sisi wenyewe tunazalisha chanjo ya kuku ambapo kuna kituo kimoja cha maabara kipo Kibaha - Dsm ambacho chanjo ya mdondo kwa dozi moja inauzwa Tshs 20,000 elfu alisema, - Mhe. Ulega.

#Kwa niaba ya Waziri wangu na Wizara yetu nataka niwachangieni ili zoezi hili na tukianza na sisi tutawapeni chanjo dozi 100,000 ili kuunga mkono jitihada zenu mjifunze na kushirikiana na AKM glitters, - Mhe. Naibu Waziri

#Tatizo la kutokuwa kwa kwa kuku ni kutokana na uhaba wa chakula bora cha kuku nataka niwahakikishie kwamba tunaenda kuratibu vizuri hili zoezi la vifaranga ili tuweze kuondokana na shida hii ya kutotolesha kiholela vifaranga vya kuku, - Mhe. Ulega

#Awali ya yote tumekubaliana lazima tudhibiti utotoleshaji wa vifafanga kiholela na utengenezaji wa vyakula vya mifugo, kuna Kampuni za kizalendo zinazohusika na uzalishaji, kampuni ya Malenga kilimanjaro, na mbezi kwa Msumi Dsm na mashamba ya kuku wazazi ambayo yanaanza kukua, pamoja na AKM, Iringa silver L. na interchick Dsm, alisema - Naibu

#Naibu alisema panashida ya vifaranga lakini tumeliona hili tatizo na tumefungua milango sasa, ambapo baada kudhibiti mipaka yetu kutokana na Operesheni Zagamba, sisi kama Wizara tumeliona hilo na tunalifanyia ufumbuzi, - Mhe. Ulega

#Tutawaunganisha na makampuni ya chakula cha kuku na tutawahamashisha vilevile, makampuni kuweka maduka ya chakula iwe rahisi kupatikana ambapo kuna Makampuni yanayohamasisha watu kufuga kuku mfano, kampuni ya malenga alieleza - Naibu Waziri.

# AKM walitoa vifaranga 4000 huko Mkuranga ambapo ilikuwa kwa mtu mmoja mmoja, ila sasa tuunde Ushirika ili uweze kusaidia kupata kwa pamoja badala ya mtu mmoja mmoja alieleza. - Naibu Waziri.

#Mhe. Ulega alisema chakula cha kuku kinapaswa kutengenezwe na maindi yenye viwango vya juu ili kiwe bora zaidi na upatikanaji wake uwe wa urahisi zaid ili kusaidia wafugaji wetu kupata chakula kwa unafuu.

#Nawakabidhini wataalamu wangu wakati wowote kutoka Wizarani ili kuwasaidia na muhakikishe mnafanya nao kazi kwa karibu sana ili Chama hiki kiweze kusonga mbele. Alimalizia kusema - Mhe. Ulega.

#Kilio kikubwa cha wafugaji wa kuku haswa ni upungufu mkubwa wa vifaranga kitaifa na wanapopatikana napo bei ni kubwa alisema hayo mlezi wa Chama hicho, Waziri Mkuu Mstaafu - Mhe. Mizengo P. Pinda.

# Vilevile uhaba wa upatikanaji wa chakula bora cha kuku kwa ajili ya ufugaji na matokeo yake wanajitokeza wauzaji feki wa vyakula, ambapo tunaomba hili liangaliwe hata ikibidi kuwe na maduka ya Serikali ambapo itakuwa rahisi na uhakika wa kupata chakula. - Mhe. Pinda

#Rai yangu kwako wewe kama Naibu Waziri mwenye dhamana ni kwamba, tutumie sisi kukuza Ushirika kwa makundi mbalmbali ya mifugo yetu ili yawe katika mfumo wa ushirika, ili iweze kuwa rahisi kusimamia, kusaidia nakuweza kutimiza malengo ya Serikali. - Mhe. pinda.

.