​​MNYETI ATETA NA VIJANA WA BBT KAGERA

Imewekwa: Tuesday 12, March 2024

MNYETI ATETA NA VIJANA WA BBT KAGERA

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Alexander Mnyeti Machi 11, 2024 amewatembelea vijana waliopo kwenye programu ya "Jenga Kesho iliyo bora kwa wajasiriamali wanawake na Vijana (BBT-LIFE) upande wa sekta ya Mifugo kwenye ranchi ya Kikulula iliyopo Karagwe mkoani Kagera.

Mbali na kukagua namna programu hiyo inavyotekelezwa kwenye ranchi hiyo Mhe. Mnyeti alifika kwenye ranchi hiyo kwa ajili ya kuzungumza na wanufaika wa programu hiyo ili kubaini kama kuna changamoto mbalimbali zinazowakabili kwenye utekelezaji wa kazi zao za kila siku.

"Mhe. Waziri amenielekeza kufika hapa na kufahamu kama kuna changamoto zozote zinazowakabili hivyo leo nahitaji kuzungumza na wanufaika hawa wa BBT tu ili nisikie kutoka kwao kama utekezaji wa azma hii ya Mhe. Rais unafanyika ipasavyo" Ameongeza Mhe. Mnyeti.

Kwa upande wao wanufaika wa programu hiyo wamepongeza hatua hiyo ya Wizara ambapo wameahidi kuendelea kutekeleza maelekezo yote wanayopewa ili waweze kuwa wajasiriamali wazuri kwa upande wa sekta ya Mifugo.

Ziara ya Mhe. Mnyeti kwa wanufaika wa programu ya "Jenga Kesho iliyo bora kwa wajasiriamali wanawake na Vijana (BBT-LIFE) upande wa sekta ya Mifugo inatarajiwa kuendelea Machi 12, 2024 ambapo atatembelea wanufaika waliopo kwenye Wakala ya Mafunzo ya Mifugo (LITA) kampasi ya Mabuki mkoani Mwanza.

.