Nifanyeje?
- Zipi sifa za kuorodheshwa kama msaidizi wa mtaalam wa mifugo? (Enlisted Paraprofessional Assistant)
- Zipi sifa za kujiandikisha kama mtaalam msaidizi wa mifugo? (Enrolled Paraprofessional).
- Daktari wa mifugo asiye mtanzania (Foreigner) anasajiliwa vipi na Baraza.
- Daktari wa mifugo asiye Mtanzania anaweza kusajiliwa na kufanyakazi hapa nchini? (Temporary and permanent registration)?
Mhe. Waziri wa mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina akipanda mti katika viwanja vya Nyakabindi Simiyu

WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI ATOA MAELEKEZO
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe.Luhaga Joelson Mpina,ametoa maelekezo kadhaa kwa Wizara ya Mifugo na Uvuvi kuyatekeleza katika kipindi cha bajeti ya Mwaka 2018/2019.
Aidha Mhe. Mpina ameelekeza yafuatayo kwa Wizara ya Mifugo na Uvuvi:Mnada wa Baridi kutoka kuwa Mnada wa Awali (Primary Market) na kuwa Mnada wa Upili (Secondary market),Kituo cha Uhimilishaji Mifugo kijengwe Simiyu na Kituo cha Uzalishaji wa Vifaranga vya Samaki pia kianzishwe Mkoani humo.
Maelekezo Mengine ni pamoja na Wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini kuwaunganisha na kuwasaidia wananchi wanaohitaji Mikopo katika Benki ya Maendelea ya Kilimo Tanzania (TADB),Makatibu Wakuu wa Mifugo na Uvuvi ndani ya siku saba wapeleke orodha ya Miradi mikubwa ya Mifugo na Uvuvi ofisi ya Waziri wa Mifugo na Uvuvi iliyokwama kwa kukosa fedha ili waweze kusaidiwa Mikopo na Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania.
Waziri Mpina alishitushwa sana na maelezo kutoka kwa afisa wa Benki ya Maendeleo ya kilimo Tanzania,Pale alipoambiwa kuwa benki hiyo ya Maendeleo ya kilimo Tanzania,Kwa Mwaka huu imeweza kukopesha wakulima (4) wanne tu kwa Mwaka mzima.
Mhe. Mpina pia aliwataka Makatibu Wakuu wa Mifugo na Uvuvi kuwaunganisha Wafugaji na Wavuvi wanaohitaji Mikopo kutoka benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania ili wafugaji,Wavuvi hao waweze kuanzisha Viwanda vya kusindika nyama,ngozi nk.ili azima ya nchi ya Viwanda iweze kufikiwa.
Waziri Mpina amemwagiza Katibu Mkuu Mifugo kueleza ni kwa nini watoa Huduma za Uhimirishaji nchini wanahimilisha Mifugo hiyo kwa bei kubwa wakati Mbegu hizo zinapatikana hapa hapa nchini na zipo chini ya Taasisi za Serikali.
Katika hatua nyingine Mhe.Mpina amewataka wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini kuweka na kukarabati Miundombinu vizuri ya Majosho,Minada na machinjio kwani kushindwa kufanya hivyo itapeleka kufuta kodi zote zitokanazo na Mazao ya Mifugo katika Halmashauri husika.
Maelekezo hayo yametolewa mkoani Simiyu alipokuwa akifanya majumuisho yake baada ya kutembelea mabanda ya waonyeshaji mbambali katika Viwanja vya Nyakabindi mkoani Simiyu.
Waziri Mpina ametaja baadhi ya changamoto zinazoikabili Sekta ya Mifugo kuwa ni pamoja na Ukosefu wa Malisho,Maji na Majosho.
"Halmashauri zote nchini zikarabati Majosho na Minanda,wasikusanye tu kodi lakini pia wakarabati Miundombinu ya Minadaa na Majosho hayo". alisema Mpina.