Mhe. Waziri wa mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina akikata utepe katika uzinduzi wa maonesho ya mifugo

Imewekwa: Tuesday 12, June 2018

Wiki ya Maziwa duniani ilianzishwa na Shirika la chakula Duniani (FAO) mwaka 2002 ambapo iliichagua wiki ya mwisho ya mwezi mei na wiki ya kwanza ya mwezi juni kila mwaka kuwa ndiyo wiki ya uhamasishaji wa unywaji wa maziwa Duniani kwa kuzingatia kuwa maziwa ni chakula bora kwa watu wa rika zote nani mlo kamili.

Kwa Tanzania utaratibu wa kuadhimisha wiki ya unywaji wa maziwa ulianzishwa na CODAFA (Chama cha wafugaji wa Ng’ombe wa Maziwa Dar es salaam) Juni 1997.Tangu mwaka 1998 hii imekuwa shughuli ya kila mwaka ikifanyika kati ya wiki ya mwisho ya mwezi meina wiki ya mwanzo ya mwezi juni.

Maadhimisho haya ya wiki ya Maziwa yalianza yakiwa na dhana ya kuhamasisha unywaji wa Maziwa na kuboresha soko la Maziwa hapa nchini,Dhana hiyo imekuwa ikibadilika na kwa sasa maadhimisho haya yanalenga kuboresha wadau wote walioko kwenye mnyororo wa thamani (Dairy value chain) kuanziamfugaji hadi mlaji.

Aidha Maadhimisho haya yanadhana ya kufungua fursa katika Sekta ya Mifugo na mazao yake na kauli mbiu ya mwaka huu 2018 ni; Fungua fursa katika Sekta ya Mifugo kwa Maendeleo ya Viwanda,”Unleashing Tanzania Livestock Potential for industrialization and Development”.

Pia Maadhimisho hayo yanamalengo kadha wa kadha kama,Kuelimisha wananchi na umma umuhimu wa maziwa katika lishe na afya bora ya binadamu.Pia kuwashawishi watunga sera umuhimu wa tasnia ya Maziwa katika kukuza uchumi wa wananchi na kuondoa Umaskini na kuwelisha wadau stadi za kuongeza ubora wa bidhaa za maziwa.

Vilevile kuwahamasishana kuwaelimisha wadau umuhimu wa kujiunga na vyama vya ushirika na kuwa na jukwaa linalowakutanisha wadau wa Tasnia ya maziwa ambapo litawawezesha kubadilishana ujuzi na uzoefu.

Akitoa taarifa kwa mgeni rasmi mwenyekiti wa wadau waTasnia ya maziwa nchini Bw. Hamisi Mzee,alisema kuwa tangu maadhimisho hayo yaanze kuadhimishwa hapa nchini sasa ni maadhimisho ya 21 tangu yalipoanza kuadhimishwa hapa tanzania mwaka 1998.Madhumuni ya maadhimisho hayo tangu mwanzo ni kuhamasisha unywaji na utumiaji wa maziwa kwa watanzania wa rika zote hasa ukizingatia kuwa Maziwa ninyenzo muhimu katika lishe ya kaya moja moja napia ni chanzo cha ajira cha kuinua uchumi wamtanzania mmojammoja na taifa kwa ujumla.

“Wadau wa tasnia ya maziwa nchini tunatumia njia mbalimbali kama vyombo vya habari,kufanya mikutano na semina mbalimbali katika kupeleka elimu kwa jamii kuelimisha umuhimu wa kutumia maziwa na na mazao yake kuwa ni lishe bora kwa afya ya binadamu”.alisema Hamisi Mzee.

Aidhamzee alisema kuwa zaidi ya nchi sitini duniani zinaadhimisha wiki ya maziwa duniani kote mei mwishoni na kuhitimishajuni mwanzoni kila mwaka,kwahiyo ufugaji wa ng’ombe wa Maziwa hauepukiki kwa sababu ni njia moja wapo ya kuondoa umaskini katika kaya za watanzania kwa kuuza maziwa mwaka mzima na kujipatia kipato,lakini pia kwa kunywa maziwa watanzania wanaimarisha afya zao.

Kwa sasa Tanzania ina ng’ombe wa maziwa milioni moja na laki moja tu (1,100,000) kiasi hiki cha ng’ombe wa maziwa ni kidogo sana, ili manufaa ya zao la maziwa na ufugaji wa ng’ombe borawa maziwa uweze kupatikanaunahitajika uwekezaji mkubwa,na kwa kuanzia Serikali imeweka mkakati wa kuzalisha ng’ombe millioni tatu (3,000,000) katika kipindi cha miaka mitano ijayo.

Ili kuweza kufikia kiwango kizuri cha uzalishaji wa maziwa,unywaji na usindika wenye ticha hapa nchini Serikali haina budi kutatua changamoto ya uhaba wa malisho,upatikanaji wa mbegu bora za malisho,na maeneo ya uzalishaji malisho yatengwe kisheria sehemu mbalimbali za wafugaji. Ingawa unywaji wa maziwa umepanda hapa nchini,kutoka lita lita 21.5 mwaka 1998 hadi kufikia lita 47.0 mwaka 2015-2017,wakati shirika la afya Duniani (WHO) limeweka kiwango cha kunywa maziwa kwa mtu mmoja kwa mwakakuwa lita 200.

.