​​MARUFUKU KUCHOMA MOTO MITUMBWI YA WAVUVI- ULEGA

Imewekwa: Wednesday 24, January 2024

MARUFUKU KUCHOMA MOTO MITUMBWI YA WAVUVI- ULEGA

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega ametoa maelekezo kwa Maafisa wanaosimamia ulinzi wa rasilimali za uvuvi kuacha kuchoma moto mitumbwi ya wavuvi iliyokamatwa kwa tuhuma za kutumika katika uvuvi haramu.

Ulega ametoa maelekezo hayo wakati akizungumza katika mkutano na Wavuvi wa Mwalo wa Magarini uliopo Wilayani Muleba, mkoani Kagera leo Januari 24, 2024.

“Zana haramu nyingine endeleeni kupambana nazo lakini mitumbwi achani kuichoma moto tafuteni njia nyingine, mbona magari na pikipiki vikikamatwa havichomwi moto”, alisema

.