Makatibu Wakuu Sekta ya Mifugo na Uvuvi (kulia) wakiteta jambo baada ya kutoka kwenye kikao cha wafanyakaz Jijini Dom

Imewekwa: Tuesday 13, November 2018

MAKATIBU WAKUU WASISITIZA USHIRIKIANO KATI YA WATUMISHI WA SEKTA YA MIFUGO NA UVUVI.

Kufuatia kikao cha watumishi Wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, kilichofanyika Leo tar 7/11/2018 katika ukumbi Wa VETA DODOMA ahamasisha yafuatayo:-

"Ushirikiano kati ya watumishi ni jambo la Msingi sana ili kuweza Kufanikisha shughuli zetu za kila siku"

" Pia ni lazima tufanye kazi kwa kujituma "

" Changamoto siyo sehemu ya maisha ila changamoto ndiyo maisha yenyewe, kwa hiyo tunazitumia hizo changamoto kama fursa."

"Wakurugenzi na wakuu Wa vitengo Jitahidini sana kuwasikiliza mnaowaongoza,na kuwasimamia na kubwa zaidi kujali maslahi yao"

"Nataka wizara hii iende kwa kasi sana,Idara ya Uzalishaji na Masoko Ikiwa kama Operating Engine kwa sababu ndiyo yenye activities nyingi sana"

"Pia napenda kuwataarifu rasmi kuwa Dr. Angelo Mwilawa kuanzia sasa nimemteua kuwa Mkurugenzi rasmi Wa idara ya Ugani na mafunzo (DRTE) hapo awali alikuwa anakaimu".

.