Nifanyeje?
- Zipi sifa za kuorodheshwa kama msaidizi wa mtaalam wa mifugo? (Enlisted Paraprofessional Assistant)
- Zipi sifa za kujiandikisha kama mtaalam msaidizi wa mifugo? (Enrolled Paraprofessional).
- Daktari wa mifugo asiye mtanzania (Foreigner) anasajiliwa vipi na Baraza.
- Daktari wa mifugo asiye Mtanzania anaweza kusajiliwa na kufanyakazi hapa nchini? (Temporary and permanent registration)?
MAGEREZA KUSAFISHA HEKTA 4000 ZA KUZALISHIA MALISHO

MAGEREZA KUSAFISHA HEKTA 4000 ZA KUZALISHIA MALISHO MSOMERA
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo) Prof. Daniel Mushi leo Machi 08, 2024 akiwa na timu ya wataalam kutoka Wizarani kwake, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Kamati ya Usalama ya Wilaya ya Handeni wametembelea na kukagua eneo litakalopandwa malisho ya Mifugo kwenye kijiji cha Msomera mkoani Tanga ambapo Jeshi la Magereza linatarajiwa kuanza kulisafisha mapema wiki ijayo.
Mradi huo wa uondoaji vichaka kwenye eneo hilo ni hatua ya awali ya uandaaji wa vitalu vitakavyozalishwa malisho ya mifugo inayoendelea kuhamishwa kutoka hifadhi ya Ngorongoro ambapo kwa kuanzia jeshi hilo linatarajiwa kusafisha hekta 2000 za awali huku nyingine zikisafishwa awamu ya pili.
"Tumekagua eneo lote na tumejiridhisha kupitia ramani ya kijiji hiki na mipaka yake na tunapenda zoezi hili lifanyike haraka ili lisiathiriwe na mvua za Masika ambapo kwa huku msimu wake ndo unakaribia" Amesema Prof. Mushi.
Tukio lililofanyika leo ni utekelezaji wa maelekezo ya Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega alilolitoa jana Machi 07, 2024 mara baada ya kufika kijijini hapo ambapo alimuelekeza Prof. Mushi kuhakikisha mradi wa usafishwaji wa eneo hilo unaanza mara moja ili wafugaji wa kijiji hicho wawe na uhakika wa malisho ya mifugo yao wakati wote.