Nifanyeje?
- Zipi sifa za kuorodheshwa kama msaidizi wa mtaalam wa mifugo? (Enlisted Paraprofessional Assistant)
- Zipi sifa za kujiandikisha kama mtaalam msaidizi wa mifugo? (Enrolled Paraprofessional).
- Daktari wa mifugo asiye mtanzania (Foreigner) anasajiliwa vipi na Baraza.
- Daktari wa mifugo asiye Mtanzania anaweza kusajiliwa na kufanyakazi hapa nchini? (Temporary and permanent registration)?
MADAKTARI 120 WA WANYAMA WAFUTIWA USAJILI

MADAKTARI 120 WA WANYAMA WAFUTIWA USAJILI
Wizara ya Mifugo na Uvuvi kupitia Baraza lake la Veterinari nchini imefuta usajili wa madaktari 120 wa wanyama na majina yao yameondolewa kwenye rejesta ya madaktari hao kutokana na kutotimiza matakwa ya kisheria.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa hivi karibuni, na Ofisi ya Msajili wa baraza hilo madaktari hao wamefutwa katika kikao kilichofanyika Tarehe 23 Mwezi Desemba 2024, kufuatia baraza kupatiwa jukumu la kusimamia wataalamu wa afya ya wanyama na utolewaji wa huduma ya afya ya wanyama nchini kwa kuwa limeundwa chini ya kifungu cha 3 cha sheria ya Veterinari, SURA 319.
Kwa mamlaka iliyopatiwa Baraza la Veterinari Tanzania kwa kifungu 25 (a), (b)(i)(ii) ya sheria ya Veterinari, SURA 319, taarifa inatolewa kwa umma na kuorodheshwa kwa majina ya madaktari hao waliofutiwa usajili kwenye tovuti ya baraza hilo www.vct.go.tz kuwa hawaruhusiwi kujihusisha na shughuli yoyote inayohusiana na utoaji wa huduma ya afya ya wanyama.
Baraza la Veterinari Tanzania linatekeleza majukumu yake likiwa chini ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi yenye dhamana ya kusimamia sekta hizo pamoja na wataalamu wanaotoa huduma kwa wananchi.