MAAFISA UGANI WATAKIWA KUHAMASISHA “GESTI ZA MIFUGO” KATIKA MAENEO YAO

Imewekwa: Monday 18, March 2024

MAAFISA UGANI WATAKIWA KUHAMASISHA “GESTI ZA MIFUGO” KATIKA MAENEO YAO

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega amewataka Maafisa Ugani kuhamasisha Gesti za mifugo kwa Wafugaji waliopo katika maeneo yao ikiwa ni moja ya hatua za kuhamasisha ufugaji wa kisasa hapa nchini.

Waziri Ulega ametoa maelekezo hayo wakati akifungua mafunzo rejea ya maafisa ugani 1000 wa nchi nzima yaliofanyika mjini Kibaha mkoani Pwani Machi 18, 2024.

“Washawishini watu wenye mashamba makubwa waliopo katika maeneo yenu waanzishe programu hii ya gesti za mifugo, tengenezeni mkakati mzuri wa kuhamasisha watu kufanya ufugaji wa kisasa kupitia gesti hizo za mifugo”, alisema

.