Nifanyeje?
- Zipi sifa za kuorodheshwa kama msaidizi wa mtaalam wa mifugo? (Enlisted Paraprofessional Assistant)
- Zipi sifa za kujiandikisha kama mtaalam msaidizi wa mifugo? (Enrolled Paraprofessional).
- Daktari wa mifugo asiye mtanzania (Foreigner) anasajiliwa vipi na Baraza.
- Daktari wa mifugo asiye Mtanzania anaweza kusajiliwa na kufanyakazi hapa nchini? (Temporary and permanent registration)?
MAAFISA UGANI WASIGEUZWE WAKUSANYA USHURU WA HALMASHAURI-MNYETI

MAAFISA UGANI WASIGEUZWE WAKUSANYA USHURU WA HALMASHAURI-MNYETI
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Alexander Mnyeti amewataka wakurugenzi wa Halmsahauri zote nchini kutowatumia maafisa ugani upande wa sekta ya Uvuvi kama sehemu ya wakusanya ushuru wa Halmashauri zao na badala yake wawaache watekeleze jukumu lao la msingi la kuwahudumia wavuvi waliopo kwenye maeneo yao.
Mhe. Mnyeti ameyasema hayo wakati wa hafla ya kugawa pikipiki 53 zenye thamani ya takribani milioni 146.5 kwa maafisa ugani wa sekta ya Uvuvi kutoka mikoa 13 nchini iliyofanyika Novemba 11, 2023 kwenye Ofisi ndogo za Wizara hiyo zilizopo jijini Dar-es-salaam.
Mhe. Mnyeti amebainisha kuwa Maafisa ugani wanapaswa kutoa elimu kwa wavuvi waliopo kwenye maeneo yao juu ya namna na nyezo sahihi wanazotakiwa kutumia wakati wa utekelezaji wa shughuli zao.
“Mnafanya kazi ya kukusanya ushuru na Halmashauri zinajisifu zimepata mapato wakati kule kwenye mialo ni fujo kubwa kati ya wavuvi na maafisa uvuvi jambo ambalo ni kinyume kabisa na lengo la Serikali kuwapeleka huko” Ameongeza Mhe. Mnyeti.
Mhe. Mnyeti ameelezea uanzishwaji wa Mamlaka ya Uvuvi nchini kama moja ya njia za kukabiliana na changamoto hiyo ambapo amaeweka wazi kuwa itawasimamia kikamilifu maafisa ugani ili waweze kutekeleza majukumu yao.
Aidha Mhe. Mnyeti amewataka Maafisa ugani hao kutumia pikipiki walizopewa kuwafuata wavuvi walipo na kwenda kuwasaidia changamoto zinazowakabili kwenye shughuli zao na kuwasisitiza wasizitumie kwa shughuli zao binafsi hasa baada ya muda wa kazi.
Akisoma taarifa fupi kabla ya makabidhiano hayo Mkurugenzi wa Utafiti, Mafunzo na Ugani kwa upande wa sekta ya Uvuvi Prof. Mohammed Sheikh amesema kuwa hitaji la maafisa ugani kwa upande wa sekta hiyo kwa nchi nzima ni 16,000 ambapo waliopo kwa sasa ni 667 pekee idadi ambayo ameweka wazi haikidhi hali ya utoaji huduma kwa wavuvi waliopo nchini.
Akizungumza kwa niaba ya maafisa ugani wenzake, Afisa Uvuvi kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Misenyi Bw. Maengo Nchimani ameishukuru Serikali kwa kuwagawia vitendea kazi hivyo ambayo anaamini vitawasaidia kuwafikia wavuvi waliopo kwenye maeneo yao kwa urahisi.
Tukio la ugawaji pikipiki kwa maafisa ugani upande wa sekta ya Uvuvi limefanyika ikiwa ni siku chache baada ya kuanza kwa zoezi la ugawaji wa boti za Uvuvi kwa wavuvi waliopo kanda ya Ziwa na bahari ya hindi hali inayoendelea kuthibitisha dhamira ya dhati ya Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuinua uchumi wa mvuvi mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.