MAAFISA UGANI PWANI NA MASHARIKI WAAHIDI KWENDA KUCHAPA KAZI!

Imewekwa: Tuesday 19, March 2024

MAAFISA UGANI PWANI NA MASHARIKI WAAHIDI KWENDA KUCHAPA KAZI!

Maafisa Ugani (Mifugo) upande wa kanda ya Mashariki na Pwani wameahidi kwenda kutekeleza kwa vitendo yale yote waliyoelekezwa kupitia mafunzo rejea yaliyofanyika Wilaya ya Kibaha mkoani Pwani kuanzia Machi 18-19, 2024.

Wakizungumza mara baada ya kufungwa kwa mafunzo hayo kwa upande wa kanda hiyo Maafisa ugani hao mbali na kuipongeza Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa kuwawezesha mafunzo hayo wamekiri kuongezewa ujuzi wa masuala mbalimbali yanayotokana na mabadiliko ya teknolojia na tabia nchi.

"Kulikuwa na mada nyingi lakini binafsi nimependa ile ya udhibiti wa magonjwa ya Mifugo kwa sababu kwa kufanya hivyo ndipo wafugaji watapata fursa nzuri ya kupata kipato kizuri lakini kinyume na hapo uchumi wa wafugaji utaendelea kushuka" Amesema Bi. Ruwaichi Elia ambaye ni Afisa Ugani wa Kata ya Maweni iliyopo Halmashauri ya jiji la Tanga.

Naye Afisa Ugani kutoka Halmashauri ya wilaya ya Kibaha Bw. Makoye Kayungilo ameonesha kuvutiwa zaidi na mada inayohusu uzalishaji wa malisho na vyakula vya Mifugo na namna ya kuvihifadhi ambapo ameahidi kwenda kuongeza ubunifu kwenye eneo lake la kazi ili kuwaongezea tija wafugaji wake.

Akizungumzia namna alivyovutiwa na dhana ya "gesti ya mifugo" Afisa Ugani kutoka Kata za Chanika na Zingiziwa zilizopo Halmashauri ya jiji la Ilala Bi. Monica Ndunguru ameweka wazi mpango wa kwenda kuitekeleza katika maeneo yake huku akitoa rai kwa wataalam wenzake kufanya kazi kwa kufuata miongozo, kanuni na utaratibu wa ufugaji bora.

Awali akitoa taarifa fupi ya namna mafunzo hayo yalivyoendeshwa, Mkurugenzi wa Utafiti, Mafunzo na Ugani Dkt. Angelo Mwilawa amesema kuwa lengo la kuendesha mafunzo hayo ni kuwanoa wataalam hao juu ya teknolojia mbalimbali za kimkakati zinazotekelezwa kupitia sekta ya Mifugo nchini kwa upande wa kosaafu za Mifugo, malisho na vyakula vya Mifugo na udhibiti wa magonjwa ya Mifugo.

"Kikubwa zaidi ni kuona namna gani sisi Maafisa ugani tunaweza kuchukua maboresho na mbinu hizi kwenda kuwafundisha wafugaji kwa wingi wao katika maeneo mbalimbali ya nchi" Ameongeze Dkt. Mwilawa.

Aidha Dkt. Mwilawa amehitimisha kwa kuwaalika wadau mbalimbali wa maendeleo kutoka sekta binafsi kuendelea kutoa mafunzo hayo kwa maafisa ugani na kushirikiana nao ili waweze kuwahudumia wafugaji ipasavyo.

Mafunzo Rejea kwa Maafisa Ugani 1000 nchi nzima kwa mwaka huu yanafanyika katika kanda mbalimbali kupitia Wilaya za Manyoni, Kaliua, Chato, Bunda, Kibaha, Masasi, Mbozi na Babati.*MAAFISA UGANI PWANI NA MASHARIKI WAAHIDI KWENDA KUCHAPA KAZI!*

Maafisa Ugani (Mifugo) upande wa kanda ya Mashariki na Pwani wameahidi kwenda kutekeleza kwa vitendo yale yote waliyoelekezwa kupitia mafunzo rejea yaliyofanyika Wilaya ya Kibaha mkoani Pwani kuanzia Machi 18-19, 2024.

Wakizungumza mara baada ya kufungwa kwa mafunzo hayo kwa upande wa kanda hiyo Maafisa ugani hao mbali na kuipongeza Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa kuwawezesha mafunzo hayo wamekiri kuongezewa ujuzi wa masuala mbalimbali yanayotokana na mabadiliko ya teknolojia na tabia nchi.

"Kulikuwa na mada nyingi lakini binafsi nimependa ile ya udhibiti wa magonjwa ya Mifugo kwa sababu kwa kufanya hivyo ndipo wafugaji watapata fursa nzuri ya kupata kipato kizuri lakini kinyume na hapo uchumi wa wafugaji utaendelea kushuka" Amesema Bi. Ruwaichi Elia ambaye ni Afisa Ugani wa Kata ya Maweni iliyopo Halmashauri ya jiji la Tanga.

Naye Afisa Ugani kutoka Halmashauri ya wilaya ya Kibaha Bw. Makoye Kayungilo ameonesha kuvutiwa zaidi na mada inayohusu uzalishaji wa malisho na vyakula vya Mifugo na namna ya kuvihifadhi ambapo ameahidi kwenda kuongeza ubunifu kwenye eneo lake la kazi ili kuwaongezea tija wafugaji wake.

Akizungumzia namna alivyovutiwa na dhana ya "gesti ya mifugo" Afisa Ugani kutoka Kata za Chanika na Zingiziwa zilizopo Halmashauri ya jiji la Ilala Bi. Monica Ndunguru ameweka wazi mpango wa kwenda kuitekeleza katika maeneo yake huku akitoa rai kwa wataalam wenzake kufanya kazi kwa kufuata miongozo, kanuni na utaratibu wa ufugaji bora.

Awali akitoa taarifa fupi ya namna mafunzo hayo yalivyoendeshwa, Mkurugenzi wa Utafiti, Mafunzo na Ugani Dkt. Angelo Mwilawa amesema kuwa lengo la kuendesha mafunzo hayo ni kuwanoa wataalam hao juu ya teknolojia mbalimbali za kimkakati zinazotekelezwa kupitia sekta ya Mifugo nchini kwa upande wa kosaafu za Mifugo, malisho na vyakula vya Mifugo na udhibiti wa magonjwa ya Mifugo.

"Kikubwa zaidi ni kuona namna gani sisi Maafisa ugani tunaweza kuchukua maboresho na mbinu hizi kwenda kuwafundisha wafugaji kwa wingi wao katika maeneo mbalimbali ya nchi" Ameongeze Dkt. Mwilawa.

Aidha Dkt. Mwilawa amehitimisha kwa kuwaalika wadau mbalimbali wa maendeleo kutoka sekta binafsi kuendelea kutoa mafunzo hayo kwa maafisa ugani na kushirikiana nao ili waweze kuwahudumia wafugaji ipasavyo.

Mafunzo Rejea kwa Maafisa Ugani 1000 nchi nzima kwa mwaka huu yanafanyika katika kanda mbalimbali kupitia Wilaya za Manyoni, Kaliua, Chato, Bunda, Kibaha, Masasi, Mbozi na Babati.

.