Nifanyeje?
- Zipi sifa za kuorodheshwa kama msaidizi wa mtaalam wa mifugo? (Enlisted Paraprofessional Assistant)
- Zipi sifa za kujiandikisha kama mtaalam msaidizi wa mifugo? (Enrolled Paraprofessional).
- Daktari wa mifugo asiye mtanzania (Foreigner) anasajiliwa vipi na Baraza.
- Daktari wa mifugo asiye Mtanzania anaweza kusajiliwa na kufanyakazi hapa nchini? (Temporary and permanent registration)?
UZINDUZI WA PROGRAMU YA KUENDELEZA SEKTA YA KILIMO AWAMU YA PILI (ASDP II)

Sekta ya kilimo ina mchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi wa
Tanzania. Asilimia 90 ya ardhi ya Tanzania hulimwa na wakulima
wadogo. Sekta inatoa ajira kwa asilimia 65.5 na huchangia asilimia 29.1
ya pato la Taifa, asilimia 30 ya soko la nje na asilimia 65 ya malighafi
za viwanda.
Ili kuendeleza sekta ya Kilimo, Serikali kupitia Wizara za Sekta ya
Kilimo (ASLMs)1 na kwa kushirikiana wa wadau wa sekta imeandaa
Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo Awamu ya pili (ASDP
II). ASDP II ni muendelezo wa awamu ya kwanza ya Programu ya
Kuendeleza Sekta ya Kilimo (ASDP I) iliyotekelezwa kuanzia 2006/2007
hadi 2013/2014. ASDP II ni mpango wa miaka kumi utakaotekelezwa
kuanzia 2017/2018 hadi 2017/2028 kwa vipindi viwili vya miaka
mitano mitano. Utekelezaji wa awamu ya kwanza utaanza 2017/2018
hadi 2022/2023. ASDP II inalenga katika kuleta mageuzi ya Sekta ya
kilimo (kilimo, mifugo na uvuvi) ili kuongeza uzalishaji na tija, kufanya
kilimo kiwe cha kibiashara zaidi na kuongeza pato la wakulima wadogo
kwa ajili ya kuboresha maisha yao, uhakika wa usalama wa chakula na
lishe, na kuchangia katika pato la Taifa.
ASDP II imeandaliwa kwa kuzingatia mikakati yote ya Taifa: Dira
ya Maendeleo ya Taifa ya 2025; Mpango wa Maendeleo wa Muda
Mrefu (2012-2021); Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2016-
2021); Mkakati wa Kuendeleza Sekta ya Kilimo (2015) na Mpango
wa Uwekezaji katika Sekta ya Kilimo (Tanzania Agriculture and Food
Security Investment Plan – TAFSIP 2011). Pia programu hii imezingatia
mambo makuu tuliyojifunza katika utekelezaji wa ASDP I ili kukabiliana
na mapungufu na changamoto za sekta ya kilimo na kuongeza kasi ya
ukuaji wa pato la Taifa, kuboresha ukuaji wa pato la wakulima wadogo
na kuwa na uhakika wa usalama wa chakula ifikapo 2025.