Nifanyeje?
- Zipi sifa za kuorodheshwa kama msaidizi wa mtaalam wa mifugo? (Enlisted Paraprofessional Assistant)
- Zipi sifa za kujiandikisha kama mtaalam msaidizi wa mifugo? (Enrolled Paraprofessional).
- Daktari wa mifugo asiye mtanzania (Foreigner) anasajiliwa vipi na Baraza.
- Daktari wa mifugo asiye Mtanzania anaweza kusajiliwa na kufanyakazi hapa nchini? (Temporary and permanent registration)?
KATIBU MKUU WIZARA YA MIFUGO NA UVUVI(MIFUGO) DKT.MARIA MASHINGO ATOA SOMO KWA WAFUGAJI KASULU

Katibu Mkuu Mifugo Dkt. Maria Mashingo amewambia wafugaji hao kuwa zoezi la usajili Mifugo sio la hiari bali ni lazima mifugo yote nchini isajiliwe kuanzia Ng'ombe wenye umri wa Miezi sita na kuendelea kulingana na matakwa ya sheria ya Utambuzi,Usajili na ufuatiliaji wa Mifugo Na. 12 ya mwaka 2010.
Awali katibu Mkuu Dkt.Maria Mashingo alikutana na mkuu wa mkoa wa Kigoma Mhe.Brigedia Mstaafu Emmanuel Maganga,na kupata taarifa ya mkoa juu ya zoezi la usajiri wa Mifugo.
Aidha Mhe Maganga amemwambia katibu mkuu kuwa zoezi linaendelea Vizuri na mwitikio ni mkubwa kutoka kwa wafugaji,taarifa ya mkoa wa kigoma inaonyesha kuwa jumla ya ng'ombe 93,182 wameshapigwa chapa kati ya Ng'ombe 345,469 waliotambuliwa ambao ni sawa na asilimia 27.
Kwa Upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Kasulu Bi.Fatima Laay amemweleza Katibu mkuu kuwa jumla ya Ng'ombe 7,552 kati ya 10,000 wenye umri wa zaidi ya miezi sita na kuendelea tayari wameshapigwa chapa ambao ni sawa na asilimia 75.52.
Aidha Bi.Laay amesema kuwa Halmashauri bado inaendelea kukusanya takwimu mbalimbali za Mifugo ambapo kila Mfugaji/Mkazi atatambulika kwa anwani,aina ya Mifugo na idadi ya Mifugo kwa ajili ya kutengeneza kanzidata (Database) ya halmashauri.