Katibu Mkuu Mifugo Prof. Elisante Ole Gabriel akishika ndama aina ya Ankole

Imewekwa: Monday 27, August 2018

KATIBU MKUU MIFUGO AFANYA ZIARA KAMPUNI YA RANCHI ZA TAIFA (NARCO).

Akitoa taarifa fupi kwa Katibu Mkuu Mifugo Prof.Elisante Ole Gabriel Bw.Mashaka Milonge,Msimamizi wa mashamba ya NARCO kanda ya Ziwa amemwambia Katibu Mkuu kuwa lengo kubwa la kuanzishwa kwa Ranchi hizo ni kufuga na kuzalisha Ng'ombe bora wa nyama aina ya Boran ambao wana ubora zaidi wa nyama,ambao hukua kwa haraka na kuvumilia mabadiliko ya tabia nchi.

Aidha Milonge ametaja lengo lingine kuwa ni pamoja na kuwauzia wafugaji wadogo madume bora ya Boran ili kuboresha Ng'ombe wa kienyeji,kuwa kichocheo cha Ufugaji bora kwa wafugaji majirani na kuwa shamba darasa juu ya Ufugaji bora wenye tija kwa Wananchi mbalimbali hapa Tanzania.

Naye Matalam wa Malisho kutoka Ranchi ya Mabale Bw.Mackanya Makanya amesema kuwa sekta ya Mifugo inamchango mkubwa katika Maendeleo ya Viwanda hapa nchini kupitia malighafi mbalimbali kama Maziwa, ngozi,nyama,Mifupa,Kwato na pembe za mifugo.

Ubora na uwingi wa malighafi hizi hutegemea zaidi aina ya malisho ya Mifugo ambayo ni chakula muhimu.Ubora na Uwingi wa Malisho ndio chazo cha Ubora na wingi wa malighafi za mifugo kwaajili ya Viwanda.

"Ili kuzingatia ubora wa Malisho kwenye nyanda za Malisho,Mfugaji anashauriwa Kuhakikisha uwepo wa Malisho yenye viwango vya juu vya virutubisho na uwepo wa Malisho jamii ya nyasi ili kupata nishati na mimea jamii ya mikunde ili kupata protini kwaajili ya mnyama pamoja na virutubisho Vingine."alisema.

Akifanya majumusho ya ziara yake katika ranchi hizo,Katibu Mkuu Mifugo amehimiza wafugaji kuhimilisha Mifugo yao kwa kutumia Mbegu bora za madume ya ng'ombe zinazozalishwa kwa njia chupa katika kituo cha Taifa cha Uzalishaji wa Mifugo (NAIC)

Prof.Ole Gabriel amesema kuwa lengo kubwa la kutembelea ranchi hizo za Missenyi,Kikurula na Mabale ni Kuhakikisha zinakuwa mfano bora wa kutoa elimu kwa wafugaji na kuboresha maisha ya wafugaji.

"Tunapozungumzia uhimilishaji tunafanya Kwanza utafiti wa Mbegu zipi zinafaa katika eneo fulani na Mbegu zipi hazifai sehemu fulani,tuna aina zaidi ya moja ya Mbegu hizi za Uhimirishaji".alisema.

Aidha katibu Mkuu amewahimiza wafugaji kutumia mbegu hizi zinazozalishwa kwa njia ya chupa kwani zinatumika kwa ng'ombe aina zote,wa kienyeji na wa kisasa,ambao wanaleta matokeo chanya kwa Uchumi wa mwananchi mmoja mmoja na kwa Taifa kwa ujumla kwani wanatoa maziwa mengi na bei yake ni rahisi, inamfikia mfugaji wa chini kabisa kwa Tsh. elfu tano (5,000) tu kwa maelekezo ya Serikali.

Pia amewataka Wananchi kufuga mifugo itakayowaletea tija,kwani NARCO kwa kushirikiana na Sekta binafsi wamejipanga kuanzisha kiwanda cha Nyama Kagera,kitakachopelekeawafugaji kupata soko la mifugo yao na hatimaye kupelekea migogoro ya wakulima na wafugaji kupungua kwa kiasi kikubwa sana.

"Serikali ya awamu ya tano Chini Rais John Pombe Magufuli imedhamilia kumaliza kabisa migogoro ya wakulima na wafugaji,ukisoma ilani ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi 2015-2020 ibara ya 25 (Q) inasema:Kuitafutia Ufumbuzi wa Kudumu Migogoro ya wakulima na Wafugaji".alisema.

Vilevile Prof.Ole Gabriel amesema Serikali imejipanga katika kutatua changamoto ya Maji na Malisho kwa Mifugo,Ilani ya cha Chama cha Mapinduzi ibara ya 25 (b) inaeleza kwamba"Itatenga na kupima na kumilikisha wafugaji maeneo ya Ufugaji nchini ili kuongeza maeneo ya Ufugaji yaliyopimwa kutoka Hekta Milioni 1.4 za sasa hadi Hekta Milioni 5.0 Mwaka 2020".alisema.

Katika hatua nyingine Katibu Mkuu Mifugo amesema kuwa Serikali kwa sasa ipo katika mazungumzo na Serikali ya Brazil ili kuleta teknolojia ya Embryo transfer (Kiini tete) hapa nchini,ambapo Mbegu ya ng'ombe dume na jike inakuwa tayari imeshaunganishwa.

Pia Prof.Ole Gabriel alipata fursa ya kukagua vitalu vya malisho mbalimbali yanayozalishwa katika ranchi ya Mabale.

.