Nifanyeje?
- Zipi sifa za kuorodheshwa kama msaidizi wa mtaalam wa mifugo? (Enlisted Paraprofessional Assistant)
- Zipi sifa za kujiandikisha kama mtaalam msaidizi wa mifugo? (Enrolled Paraprofessional).
- Daktari wa mifugo asiye mtanzania (Foreigner) anasajiliwa vipi na Baraza.
- Daktari wa mifugo asiye Mtanzania anaweza kusajiliwa na kufanyakazi hapa nchini? (Temporary and permanent registration)?
Katibu Mkuu Mifugo Prof. Elisante akiwa ameshika Liquid Nitrogen

KATIBU MKUU MIFUGO AHAMASISHA WAFUGAJI KUFUGA KISASA ILEMELA MWANZA.
Katibu Mkuu Mifugo Prof.Elisante Ole Gabriel amewataka wafugaji nchini kufuga kisasa ili waweze kujikwamua na Umaskini na kuongeza kipato.
Hayo ameyasema leo alipokuwa katika ziara ya Mikoa sita (6) jijini mwanza ikiwemo,Geita,Simiyu,Mara,
Akiongea na wafugaji katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela Katibu Mkuu Mifugo amesema kuwa lengo kubwa la ziara yake ni kutambua changamoto zinazowakabili wafugaji nchini na kuzitafutia ufumbuzi,kuhamasisha wafugaji kukubali uhimilishaji wa Mifugo yao na kuangalia namna bora ya utatuzi wa changamoto ya Malisho.
Changamoto nyingine aliyoitaja ni pamoja na Ukosefu wa Masoko wa bidhaa za Mifugo na changamoto ya wafugaji kuwa na mwitikio kidogo juu Ufugaji wa kisasa.
Aidha Prof.Ole Gabriel amesema kuwa changamoto hizo zote zitatatuliwa kwasababu Serikali ya awamu ya Tano Chini ya Rais Mahili John Pombe Magufuli imedhamili kutatua changamoto hizo kwani ukisoma Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ibara ya 25 (a)- (Q) inaeleza waziwazi juu ya utatuzi wa changamoto hizo.
Pia prof.Ole Gabriel ameongeza kuwa changamoto ya upatikana wa mbegu bora kwa ajili ya Uhimilisha kuuzwa kwa bei kubwa sasa changamoto hiyo itapatiwa ufumbuzi kwani Serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi itasafirisha hizo Mbegu mkoa wowote utakao hitaji kwa gharama ya Tsh 3, 000/= mpaka mkoa husika na Wananchi wauziwe bei ya Tsh. elflfu tano (5,000) tu.
"Hizi Mbegu za madume bora zinauzwa elfu Hamsini,lakini Serikali ya awamu ya tano imebeba jukumu hilo na kupunguza bei hiyo mpaka kufikia Tsh 3,000/= kwa chupa na impaka inamfikia Mfugaji wa chini kabisa isiuzwe zaidi ya elfu tano". alisema.
Mtungi Mkubwa wa Lita 35 wa Liquid Nitrogen wa kuhifadhia Mbegu hizo unauzwa.Tsh.1,750, 000/=na mtungi mdogo wa Lita tatu Unauzwa 750,000/=hivyo,katibu mkuu Mifugo ametoa rai kwa mikoa na Halmashauri zote hapa nchini inunue mitungi hiyo ya liquid na nitrogen.
"Uzuri wa mbegu hizi ni kwaajili ya Uhimirishaji wa ng'ombe aina zote,wa kienyeji na Maziwa pia"alisema
Awali Prof.Ole Gabriel alitoa wito kwa Makatibu Tawala wa Mikoa (RAS) wote Tanzania Kuhakikisha wananunua mitungi mikubwa ya LiQuid Nitrogen katika mikoa yao ili iwe rahisi katika utunzaji wa Mbegu za madume bora.kwa ajili ya Uhimilishaji