Nifanyeje?
- Zipi sifa za kuorodheshwa kama msaidizi wa mtaalam wa mifugo? (Enlisted Paraprofessional Assistant)
- Zipi sifa za kujiandikisha kama mtaalam msaidizi wa mifugo? (Enrolled Paraprofessional).
- Daktari wa mifugo asiye mtanzania (Foreigner) anasajiliwa vipi na Baraza.
- Daktari wa mifugo asiye Mtanzania anaweza kusajiliwa na kufanyakazi hapa nchini? (Temporary and permanent registration)?
KAMATI YAVUTIWA NA UZALISHAJI WA MALISHO SHAMBA LA VIKUGE

KAMATI YAVUTIWA NA UZALISHAJI WA MALISHO SHAMBA LA VIKUGE
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya viwanda , Biashara ,Kilimo na Mifugo imeridhishwa na kazi ya uzalishaji wa mbegu za malisho ya mifugo katika shamba la serikali lililopo katika kijiji cha vikunge wilaya ya Kibaha mkoani Pwani.
Akizungumza baada ya kukagua Shamba hilo, mapema leo Machi 19, 2024, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Deogratus Mwanyika amesema kamati yake imeridhishwa na ubora wa mbegu zinazozalishwa katika shamba hilo na kuiomba wizara ya mifugo ianze kusambaza mbegu hizo kwa wafugaji katika maeneo mbalimbali ili wakaanzishe mashamba ya malisho ambayo watayatumia kulishia mifugo yao wakati wa kiangazi.
Awali akiikaribisha kamati hiyo Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega ameihakikishia kamati hiyo kwamba kwa sasa suala la uanzishwaji wa mashamba ya malisho nchini ndio kipaumbele na kuwaomba wajumbe wa kamati hiyo kuwa mabalozi wa kuhamasisha wananchi kulima malisho kwa ajili ya mifugo yao.