DKT. MHEDE ANADI UFUGAJI SAMAKI KWA NJIA YA VIZIMBA

Imewekwa: Saturday 21, December 2024

  1. DKT. MHEDE ANADI UFUGAJI SAMAKI KWA NJIA YA VIZIMBA

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Dkt. Edwin Mhede ameendelea kuhamasisha ufugaji wa samaki kwa njia ya Vizimba kwa wanachi wa Wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza.

Dkt. Mhede amebainisha hayo wakati wa ziara yake aliyoifanya Wilayani humo leo Disemba 21, 2024 ambapo alitembelea mialo ya Nyakaliro na Kanyala kwa lengo la kuona namna inavyofanya kazi.

"Kwenye Halmashauri kuna ile mikopo ya asilimia 10 ambayo siwezi kuwapangia matumizi lakini kama mnavyoona hali yetu ya Upatikanaji samaki kwa sasa umepungua na Halmshauri yenu asilimia kubwa ya mapato mnaipata kwenye kupitia shughuli za Uvuvi hivyo naamini ufugaji samaki utawalipa zaidi" Amesema Dkt. Mhede.

Akiwa kwenye mualo wa Kanyala unaomilikiwa na Mfanyabiashara wa Samaki Bw. Selemani Mbuga Dkt. Mhede amempongeza mdau huyo wa Uvuvi na kuwataka wengine kuiga mfano huo ili kuendelea kuchagiza maendeleo ya sekta ya Uvuvi nchini.

"Hata sisi umetupa changamoto kwa sababu tunahitaji kuweka mialo ya kushushia samaki wanaotoka kwenye vizimba vyetu" Ameongeza Dkt. Mhede.

Aidha Dkt. Mhede ametumia ziara hiyo kuwasihi wananchi wa Wilaya hiyo kushirikiana na Serikali katika mapambano dhidi ya Uvuvi haramu ili kuendelea kulinda rasilimali za Uvuvi zilizopo Ziwa Victoria.

.