TARATIBU ZA KUSAFIRISHA MIFUGO NDANI NA NJE YA NCHI

1. KUTOKA KWA WATU BINAFSI

Nyaraka muhimu wakati wa kusafirisha Mifugo kutoka kwa mtu binafsi:- Uthibitiso/Kibali cha uhalali wa Umiliki wa Mifugo  Kibali cha hali ya Afya ya Mifugo (Livestock Health Certificate)  Kibali cha kusafirishia Mifugo (Livestock Movement Permit).

2. KUTOKA KATIKA MINADA YA MIFUGO

Nyaraka muhimu wakati wa kusafirisha Mifugo kutoka Minada ya Mifugo:- 

Leseni ya kufanya biashara ya mifugo ndani au nje ya nchi; 

Malipo ya Ushuru wa Mnadani (Market fee); 

Cheti cha hali ya Afya ya Mifugo (Livestock Health Certificate)  Kibali cha kusafirishia Mifugo (Livestock Movement Permit).

3. KWENDA NJE YA NCHI

Nyaraka muhimu wakati wa kusafirisha Mifugo kutoka kwenda nje ya Nchi:- 

Leseni ya kufanya biashara ya Mifugo nje ya nchi; 

Kibali cha ruhusa ya kuingiza mifugo kwenye nchi inapopelekwa mifugo (importation permit); 

Kibali cha Hali ya Afya ya Mifugo (Livestock Health Certificate);  Uthibitisho wa Malipo ya Ushuru wa Mnadani (Market fee); 

Uthibitisho wa Malipo ya ushuru wa kusafirisha Mifugo nje ya nchi (Exportation Fee) 

Kibali cha Kusafirisha Mifugo nje ya nchi (Export permit)