Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Mifugo na Uvuvi

WAZIRI DKT. BASHIRU AKAGUA MRADI WA KITOTOLESHI MTWARA

Imewekwa: 15 November, 2026
WAZIRI DKT. BASHIRU AKAGUA MRADI WA KITOTOLESHI MTWARA

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa, leo Tarehe 13 Novemba 2026, ametembelea na kukagua Mradi wa Ujenzi wa Kituo cha Vitotoleshi vya Vifaranga vya Samaki katika eneo la Msimbati Mkoani Mtwara kwa lengo kuangalia maendeleo ya mradi huo utakaosaidia kupunguza tatizo la upungufu wa vifaranga.

Baada ya kukagua mradi huo, Mhe. Balozi Dkt. Bashiru ameelekeza kukamilishwa kwa kazi zilizosalia ili mradi huo uanze kufanya uzalishaji wa vifaranga vya samaki, pia amemwagiza Mkurugenzi wa Ukuzaji Viumbe Maji Nchini Kuwasilisha ripoti kuhusu maendeleo ya mradi huo.

Katika hatua nyingine Mheshimiwa Waziri amekagua mradi wa ufugaji wa samaki kwa njia ya mabwawa kupitia  vikundi vya vijana na kina mama vya Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara na Manispaa ya Mikindani mkoani Mtwara, mradi ambao unagharimu takribani Milioni 800 lakini  mradi huo kumwama kuanza uzalishaji wa samaki.

Baada ya kukagua na kuonyesha  kutoridhishwa na mradi huo, Mhe. Balozi Dkt. Bashiru ameagiza Wakala wa  Mafunzo ya Uvuvi Tanzania na Idara ya Utafiti, Mafunzo na Huduma za Ugani kufika Katika maeneo ya mradi huo kufanya tathmini, kutoa elimu kwa wanufaika na kuufufua mradi huo.

Katika ziara yake pia, ametembelea Kituo cha Hifadhi ya Bahari ya Ghuba ya Mnazi ya Mkoani Mtwara ambayo ipo chini ya Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu (MPRU).

Mrejesho, Malalamiko au Wazo