ULEGA-HUU NI MWAKA WA MATOKEO

Imewekwa: Thursday 04, July 2024

ULEGA: “HUU NI MWAKA WA MATOKEO”

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega ameitaka menejimenti ya wizara kuhakikisha katika mwaka wa fedha 2024/25 kila mmoja katika nafasi yake anawajibika ipasavyo ili utekelezaji wa miradi uwe na matokeo ya kupigiwa mfano.

Mhe. Ulega amesema hayo wakati wa kikao baina yake na Menejimenti ya Sekta ya Mifugo kilichofanyika jijini Dar es Salaam Julai 2, 2024.

“Ndugu zangu, huu ni mwaka wa kuleta matokeo, ni mwaka wa kazi, ni mwaka wa mchakamchaka, kila mmoja awajibike kwa nafasi yake katika utekelezaji wa miradi yetu ili matokeo yaonekane”, amesema

Pamoja na mambo mengine kikao hicho kilikuwa na lengo la kujadili taarifa ya mpango wa utekelezaji wa miradi iliyopangwa kutekelezwa na sekta ya mifugo katika mwaka wa fedha 2024/2025. Mheshimiwa Ulega amewata kuanza utekelezaji wa bajeti hiyo mara moja.

.