Ulega apokea mkataba kutoka kwa Mwakilishi wa Jumuiya ya Ulaya ( EU )

Imewekwa: Thursday 27, September 2018

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe Abdallah Hamis Ulega amekabidhi boti
mbili za doria kwa BMU za Kilwa Kivinje na Mafia. Zoezi hili limefanyika
katika Wilaya ya Kilwa eneo la Kivinje. Boti hizo zina thamani ya fedha za
Kitanzania milioni 144 ambazo zimefadhiliwa na Umoja wa Ulaya kupitia
miradi ya WWF.
Mwakilishi wa Umoja wa Ulaya Bibi Jenny amesema wanafadhili miradi ya
WWF hapa Tanzania yenye jumla ya bilioni 7 za Kitanzania. Aidha, amefurahi
kusikia kwa uvuvi wa mabomu umepungua sana na hii ni sababu ya juhudi za
serikali na wananchi wa maeneo haya. Pia alisema wao wamenunua boti ila
jukumu za kuzilinda ni la Serikali ya Wilaya husika.
Naye Mkurugenzi wa WWF nchini amesema wamepata taarifa kutoka kwa
wavuvi kwamba sasa samaki wanaongezeka na kupatikana kwa samaki
ambao walishapotea na haya yote ni kwa sababu ya kupungua kwa asilimia
kubwa uvuvi wa mabomu.
Mhe Ulega Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi amesema Umoja wa Ulaya
umenunua hizi boti kuunga mkono kati kubwa inayofanywa na Mhe Rais John
Pombe Magufuli ya Serikali yake ya awamu ya tano. Alisema amezunguka
wilaya za Mkinga, Tanga Mjini, Muheza, Pangani na Lindi kote huko wavuvi
wanakiri samaki wameongezeka kwa sasa.
Ukanda huu wa Pwani hauna viwanda vya samaki na kumuomba Mwakilishi
wa Umoja wa Ulaya kutafuta wawekezaji kuja kuwekeza viwanda vya samaki
katika mwambao wa bahari ya Hindi, pia alimuomba kufadhili ujenzi wa soko
la samaki Kilwa Kivinje. Mhe. Ulega aliwaasa umoja wa vikundi vya BMU
kutunza boti hizo na kuwaagiza Wilaya kusimamia ulinzi wa boti hizo. Mwisho
aliwaomba WWF kuwaangalia BMU na wavuvi wa maeneo mengine kama
Mkinga, Pangani, Lindi Vijijini na Mkuranga kwani nao wana mahitaji ya boti
kama hizi katika ulinzi wa rasilimali zetu za bahari.

.