ULEGA AITAKA NHC KUTUMIA MALIGHAFI ZA NDANI

Imewekwa: Wednesday 07, February 2024

ULEGA AITAKA NHC KUTUMIA MALIGHAFI ZA NDANI

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega amelitaka Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) ambaye ndio Mkandarasi wa ujenzi wa jengo la Ofisi za Wizara ya Mifugo na Uvuvi linalojengwa katika mji wa Serikali, Mtumba, jijini Dodoma kuhakikisha wanatumia malighafi zinazozalishwa na viwanda vilivyopo hapa nchini.

Ulega ametoa maelekezo hayo alipofanya ziara ya ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa jengo hilo leo Januari 7, 2024 ambapo aliambatana na timu ya Wataalamu wa Wizara.

“Nimekagua hapa nimeona vipo vinavyozalishwa hapa nyumbani na nyinyi ni shirika la kizalendo lakini ajabu sana mmeacha kununua vitu vya hapa nyumbani mmeamua kwenda kununua vilevile ambavyo vinapatikana hapa nchini, na mkumbuke hamjengi nyumba ya mtu binafsi ni ya umma”, alisema

Mhe. Ulega ametoa rai kwa shirika hilo kama wanachofuata huko nje ni ubora au mtindo, wakutane na wazalishaji waliopo hapa nchini na kuwaelekeza ubora na mitindo wanayoitaka ili waweze kuzalishiwa.

.