TANZANIA YASHIRIKI JUKWAA LA DUNIA LA MAEDELEO YA BAHARI
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa, amewasili katika Jiji la Qingdao nchini China kuhudhuria Jukwaa la Kidunia la Maendeleo ya Bahari (Global Ocean Development Forum) linafanyika kuanzia leo Septemba 16 hadi 18, 2026, ambapo ataiwakilisha Tanzania Katika jukwaa hilo kujadili fursa za Bahari Kuu.
Mhe. Balozi Dkt. Bashiru anashiriki Jukwaa hilo baada ya kupata mwaliko kutoka Kituo cha Taifa cha Utafiti wa Bahari Kuu ( National Deep - Sea Center), cha Jamhuri ya Watu wa China lengo ni kuimarisha ushirikiano wa kimataifa na ubadilishanaji wa Maarifa katika sekta ya Bahari na Uchumi wa Buluu.
Vile vile , Jukwaa hilo linawakutanisha wawakilishi kutoka Umoja wa Mataifa, Mamlaka ya Masuala ya Bahari za Nchi za Pwani, Viongozi wa Mashirika ya Kimataifa yanayohusiana na masuala ya bahari , wataalam mashuhuri, wasomi, wajasiriamali na wadau wa sekta ya bahari.
Baada ya kuwasili katika Jiji la Qingdao ametembelea na kujionea shughuli zinazofanywa na Taasisi ya Kwanza ya Oceanografia ya china, pamoja na kutembelea Makumbusho ya Utafiti wa Bahari ya China.